Mfanyakazi wa Barrick,Safarani Msuya akipokea cheti cha ushiriki kutoka kwa Katibu Tawala wa wilaya ya Serengeti,Angelina Marco
Wafanyakazi wa kampuni ya Barrick nchini kupitia klabu zao za mchezo wa Marathon wameshiriki katika mbio za kilomita 12 za Serengeti Anti-poaching Run 2024 zilizofanyika wilayani Serengeti mkoani Mara.
Wakimbiaji kutoka Barrick Runners clubs wamekuwa wakishiriki marathon mbalimbali zinazofanyika nchini na nje ya nchi.
Kampuni imekuwa na programu za mazoezi kwa ajili ya wafanyakazi wake kwa ajili ya kuhakikisha wanakuwa na nguvu na afya bora pia imewekeza katika miundombinu ya michezo na mazoezi kwa ajili ya kuwawezesha wafanyakazi wake kushiriki michezo na mazoezi katika mazingira rafiki.
Wafanyakazi wa Barrick wakifurahi baada ya kumaliza mbio za Serengeti Anti-poaching Run 2024
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
إرسال تعليق