Na Derick Milton, Mwanza.
Benki ya NMB inaendesha kampeni ya
‘MastaBata la Kibabe’ kuanzia Novemba 9 mwaka huu hadi Februari 12, mwakani,
ikilenga pamoja na mambo mengine, kurahisisha ulipaji ada kwa wateja wake
wanaosoma au kusomesha.
Kiasi cha Sh. million 300 kimetengwa
kwa ajili ya Kampeini hiyo, ambapo washindi wa kulipiwa ada watapokea Sh
million 4 kila mmoja.
MastaBata la Kibabe’ inahusisha pia
utoaji wa zawadi za viwango tofauti vya fedha taslimu, pamoja na kugharamia
safari za mapumziko kwa washindi, kwenda katika mbuga za wanyama hapa nchini
ambazo ni Mikumi na Ngorongoro, pamoja na (kwenda) nchini Dubai.
Ilifahamika zaidi kwamba kila
mshindi wa kwenda mapumzikoni ana fursa ya kuchagua ama kwenda mwenza
wake, ndugu au rafiki, wote wakigharamiwa kila kitu.
Vigezo vya kuwa mshindi ni kutumia
Kadi ya NMB kufanya malipi mbalimbali, alisema Mkuu wa Matawi na Mauzo Benki ya
NMB Donatus Richard, jana jijini Mwanza wakati wa kuchezesha droo ya
kupata washindi wa mwezi wa kwenda Mikumi, fedha taslimu shilingi 500,000
pamoja na zawadi ya kulipiwa ada hadi milioni nne.
“Kwa maneno mengine hii tunasema ni
‘kula bata tunakulipia ada’. Mbali na kwenda mapumzikoni au kulipiwa ada, faida
nyingine ya Kampeini hii ni kupata mitaji ya biashara kupitia zawadi wa fedha
taslimu, ikiwemo Shilingi 500,000 kwa kila mshindi.
“Lakini pia tunahamasisha matumizi
ya kadi za NMB kwa lengo la kulinda usalama wa fedha za wateja wetu.
Kutembea na fedha taslimu ni gharama kwa sababu mteja anaweza kuzipoteza kwa
namna yoyote ile, ikiwemo kuibiwa, “alisema na kufafanua zaidi kwamba:
Kigezo ni kutumia kadi ya Benki ya
NMB na sio mashine ya kadi kutoka katika Benki hiyo. Hivyo, hata mteja akifika
mahala ambapo hakuna mashine ya Benki, bado anaweza kulipia kwa mashine
nyingine yoyote na akaingia katika droo ya kuwa mshindi wa zawadi hizo.
Aliongeza kwamba hadi sasa,
takribani Sh million 34.7 zimeshatolewa kwa wasindi wapatao 333, huku
wateja 122 wakipokea zawadi mbalimbali za papo kwa papo.
Kwa ujumla, alisema, kiasi
kilichotengwa kwa ajili ya kampeini hiyo kimelenga zaidi ya washindi 2,000,
ambapo kila wiki washindi 100 watapokea Sh 100,000, washindi 40 zawadi za papo
kwa papo, 30 watajinyakulia Sh 500,000 kila mwisho wa mwezi kwa muda wa
miezi miwili, na 10 watashinda safari za kutembelea mbuga za wanyama.
“Kadhalika washindi 10 watazawadiwa
ada ya shule na washindi sita tiketi za kwenda Dubai kwa muda wa siku tano. Hii
ndio maana halisi ya ‘MastaBata la Kibabe’, alisema.
Meneja mwandamizi wa Kitengo cha
Kadi NMB, Manfred Mayala, aliwataka wananchi kujiunga na Benki hiyo ili
kunufaika na huduma mbalimbali muhimu, ikiwemo zawadi zinazotolewa kipjndi hiki
cha‘MastaBata la Kibabe’.
“Kila mtanzania ni mteja wetu. Cha
kufanya hapo ni kujiuga na Benki yetu,” alisema.
Mwakili wa Bodi ya michezo ya
kubahatisha nchini, Winfrida Kabuje, alisema mchakato wa kuwapata washindi wa
kampeini hiyo utafanyika kwa uwazi na haki, kama sheria zinavyoelekeza.
إرسال تعليق