Mradi wa EpiC Kupitia FHI 360 Wakabidhi Vifaa Kudhibiti VVU Shinyanga

Sehemu ya vifaa vilivyotolewa na Mradi wa EpiC unaotekelezwa na FHI 360 kwa ajili ya vituo vya afya na Mabinti balehe na wanawake Vijana
Kaimu Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga, Getrude Eusebio Saleko (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha vifaa vilivyotolewa na Mradi wa EpiC unaotekelezwa na FHI 360 kwa ajili ya vituo vya afya na Mabinti balehe na wanawake Vijana walioko nje ya shule Mkoani Shinyanga wanaonufaika na mradi wa EpiC.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mradi wa Meeting Targets and Maintaining Epidemic Control (EpiC) unaotekelezwa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kwa ufadhili wa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani (PEPFAR) kupitia Serikali ya Watu wa Marekani (USAID), umekabidhi vifaa vyenye thamani ya Shilingi Milioni 63 kwa ajili ya vituo vya afya na Mabinti balehe na wanawake Vijana (AGYW) wenye umri wa miaka 15-24 walioko nje ya shule Mkoani Shinyanga wanaonufaika na mradi wa EpiC.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa  Jumatano Desemba 18,2024 na Kaimu Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga, Getrude Eusebio Saleko kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha.

Akikabidhi vifaa hivyo, Getrude amesema mwaka huu 2024 mradi wa EpiC umetoa kabati za kuhifadhia kumbukumbu za wapokea huduma, computer , printer, vyerehani , mashine za kushonea masweta , majora ya vitambaa na kifaa cha kuosha na kukausha nywele kwenye saloon.
"Vifaa hivi vina thamani ya Tsh. 63,060,000/=na vitaenda kutumika katika vituo vya kutolea huduma za afya katika halmashauri zote za wilaya mkoani Shinyanga , na nyenzo hizi pia zitasaidia Mabinti balehe na wanawake Vijana wenye umri wa miaka 15-24 walioko nje ya shule kujiinua kiuchumi na vyote vitafungwa kwenye karakana za mafunzo kwa vitendo za mradi wa EpiC",amesema Getrude.

"Mwaka 2021 EpiC kupitia Afua ya DREAMS ilianzisha karakana 16 za mafunzo kwa vitendo kwa ajili ya mabinti kupata ujuzi wa kazi za mikono bila malipo. Karakana hizi zinatoa ujuzi kama kushona nguo, mafunzo ya awali ya computer, na ujuzi wa kutengeneza nywele za kike(saloon). Jumla ya mabinti 1,289 waliunganishwa katika karakana hizo za ushonanji, na mabinti 1072 waliweza kuhitimu katika ujuzi wa ushonaji, 458 walijifunza computer na 309 walihitimu mafunzo hayo, baada ya mafunzo haya jumla ya mabinti 129 walifanikiwa kupata ajira",ameongeza Getrude.
Kaimu Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga, Getrude Eusebio Saleko.

Amebainisha kuwa, kila mwaka EpiC huunga mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kuhakikisha miundombinu ya afya inaboreshwa wakati wa utekelezaji wa shughuli zake.

"Tunashukuru wadau na Serikali kwa ushirikiano wanaouonesha,  tunaahidi kuendelea kushirikiana nao bega kwa bega ili kuweza kufikia malengo ya mkoa kwenye huduma za VVU na UKIMWI",ameongeza.

Ameeleza kuwa Mradi wa EpiC unatekeleza pia Afua ya DREAMS inayohusisha Mabinti balehe na wanawake Vijana (AGYW) wenye umri wa miaka 15-24 walioko nje ya shule ambapo katika mkoa wa Shinyanga Afua ya DREAMS inahusisha halmashauri za wilaya zote 5, Ushetu, Msalala, Kahama, Shinyanga,na Manispaa ya Shinyanga.

Getrude  amebainisha kuwa katika kuendelea na udhibiti wa VVU na UKIMWI, mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na shirika la FHI 360 linalofadhiliwa na PEPFAR kupitia USAID linatekeleza mradi wa EpiC katika halmashauri 60 ndani ya mikoa 11 ya Tanzania bara ambapo kwa Mkoa wa Shinyanga, mradi huo ulianza Machi 2020 na utaendelea mpaka Septemba 2025 ukitekelezwa katika Halmashauri tano kupitia Asasi za kiraia ya SHDEPHA+ katika halmashauri za wilaya za Shinyanga, Msalala na Manispaa ya Shinyanga. Pia HUHESO Foundation inatekeleza mradi katika Halmashauri ya wilaya ya Ushetu na Manispaa ya Kahama.

Mradi huo una malengo ya utoaji wa elimu juu ya VVU, jinsi ya kujikinga ili kuzuia maambukizi mapya, mabadiliko ya tabia hatarishi na upimaji wa VVU ngazi ya jamii. Sambamba na hilo mradi unatoa mafunzo rasmi na kazini kwa watoa huduma za afya kulingana na taratibu za Serikali.

Amefafanua kuwa, katika miaka mitatu iliyopita, mradi huo umefanikiwa kufikia takribani mabinti 122,73 katika jamii kupitia huduma za kitabibu na uwezeshwaji wa kiuchumi,  kwenye huduma za kitabibu jumla ya mabinti 42,641 walipimwa maambukizi ya VVU na kati yao 524 waligundulika kuwa na maambukizi ya VVU na 438 waliweza kuanzishiwa dawa za ARV.

Kwenye huduma za kiuchumi mradi umefanikiwa kuunda na kuwezesha vikundi 1392, vyenye jumla ya mabinti 32,482, vikundi hivi viliweza kuweka akiba ya pesa za kitanzania shilingi 423,463,800/=pia mradi umeweza kupeleka mabinti158 katika mafunzo ya ufundi VETA, 30 walipata ufadhili ya EpiC na kupewa vitendea kazi baada ya mafunzo na 128 waliunganiushwa na EpiC kwa wadau wengine ikiwemo ofisi ya Mbunge Msalala.

"EpiC kwa kushirikiana na Serikali iliweza kuunganisha vikundi vya mabinti vitano na kupokea mikopo ya Serikali yenye thamani ya shilingi 47,000,000/=. Pia Mradi umewawezesha mabinti 1482 kupata kadi za NIDA, 2184 CHF cards, na vyeti vya kuzaliwa 1497",ameeleza.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha

Akipokea vifaa hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ameupongeza Mradi wa EpiC unaotekelezwa na Shirika la FHI 360 kwa ufadhili wa PEPFAR kupitia USAID kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuchangia na kusaidiana na serikali katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI kwa makundi yaliyoko kwenye hatari za kupata maambukizi ya VVU hasa mabinti.

"Tunawashukuru kwa kuwawezesha vijana hawa kiuchumi ili kudhibiti mambukizi ya VVU kwa sababu miongoni mwa sababu zinazochangia kuwepo kwa maambukizi ni umaskini, kutokuwa na kazi ya kufanya, kutotamani kufanya kazi na kuwa na tamaa matokeo yake unajiingiza katika mazingira na tabia hatarishi, vifaa hivi vitawasaidia kujiongezea kipato",amesema Macha.

"Afya ndiyo mtaji wa kila kitu na naomba mtambue kuwa UKIMWI bado upo na maambukizi sasa ni 5.6% mkoa wa Shinyanga, lazima tuendelee kuchukua hatua, tunao wajibu wa kupambana na maambukizi ya VVU, tupime afya zetu na kama una maambukizi huduma za matibabu zipo",ameongeza Macha.

Aidha ameyataka mashirika yasiyo ya kiserikali kuhakikisha yanafikia jamii na kutoa elimu ya kutosha ili kupunguza changamoto zinazowakumba wasichana, ikiwa ni pamoja na mimba za utotoni, ukatili wa kijinsia, na maambukizi ya VVU, akisisitiza kuwa serikali itaendelea kushirikiana nao ili kuunda jamii inayomthamini mtoto wa kike na kumlinda ipasavyo.
Kaimu Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga, Getrude Eusebio Saleko (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha vifaa vilivyotolewa na Mradi wa EpiC unaotekelezwa na FHI 360.

Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Rad. Faustine Mlyutu ameushukuru Mradi wa EpiC kupitia FHI 360 kwa kuwapatia vifaa hivyo na kuthamini mabinti na kuwapatia elimu ya mabadiliko ya tabia, VVU na UKIMWI, ujasiriamali na uwezeshaji kiuchumi (kuweka akiba na kukopa) kupitia vikundi vya wasichana vinavyosimamiwa na Shirika la FHI 360.

Nao wanufaika wa mradi huo akiwemo, Mbuke Daudi, Mhoja Philipo na Deniza  Paschal wameishukuru serikali na Mradi wa EpiC kwa kuwabadilisha tabia na kiuchumi wakieleza kuwa watatumia vifaa hivyo vikiwemo vyerehani , mashine za kushonea masweta , majora ya vitambaa na kifaa cha kuosha na kukausha nywele kwenye saloon kwa ajili ya kujiinua kiuchumi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza Desemba 18,2024 wakati akipokea vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 63 vilivyotolewa na Mradi wa EpiC unaotekelezwa na FHI 360 kwa ajili ya vituo vya afya na Mabinti balehe na wanawake Vijana (AGYW) wenye umri wa miaka 15-24 walioko nje ya shule Mkoani Shinyanga wanaonufaika na mradi wa EpiC. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza  wakati akipokea vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 63 vilivyotolewa na Mradi wa EpiC unaotekelezwa na FHI 360 kwa ajili ya vituo vya afya na Mabinti balehe na wanawake Vijana Mkoani Shinyanga 
 
Kaimu Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga, Getrude Eusebio Saleko akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa vilivyotolewa na Mradi wa EpiC unaotekelezwa na FHI 360 kwa ajili ya vituo vya afya na Mabinti balehe na wanawake Vijana mkoani Shinyanga.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Rad. Faustine Mlyutu akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa vilivyotolewa na Mradi wa EpiC unaotekelezwa na FHI 360 kwa ajili ya vituo vya afya na Mabinti balehe na wanawake Vijana mkoani Shinyanga.
Kaimu Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga, Getrude Eusebio Saleko (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha vifaa vilivyotolewa na Mradi wa EpiC unaotekelezwa na FHI 360 kwa ajili ya vituo vya afya na Mabinti balehe na wanawake Vijana walioko nje ya shule Mkoani Shinyanga wanaonufaika na mradi wa EpiC.
Kaimu Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga, Getrude Eusebio Saleko (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha vifaa vilivyotolewa na Mradi wa EpiC unaotekelezwa na FHI 360 kwa ajili ya vituo vya afya na Mabinti balehe na wanawake Vijana walioko nje ya shule Mkoani Shinyanga wanaonufaika na mradi wa EpiC. (Aliyelala ni mmoja wa wanufaika wa mradi wa EpiC akiwa amelala katika kifaa cha kuosha na kukausha nywele kwenye saloon)
Kaimu Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga, Getrude Eusebio Saleko (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha vifaa vilivyotolewa na Mradi wa EpiC unaotekelezwa na FHI 360 kwa ajili ya vituo vya afya na Mabinti balehe na wanawake Vijana walioko nje ya shule Mkoani Shinyanga wanaonufaika na mradi wa EpiC.
Kaimu Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga, Getrude Eusebio Saleko (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha vifaa vilivyotolewa na Mradi wa EpiC unaotekelezwa na FHI 360 kwa ajili ya vituo vya afya na Mabinti balehe na wanawake Vijana walioko nje ya shule Mkoani Shinyanga wanaonufaika na mradi wa EpiC.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akimkabidhi Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze kwa niaba ya wakurugenzi wa Halmashauri vifaa vilivyotolewa na Mradi wa EpiC unaotekelezwa na FHI 360 kwa ajili ya vituo vya afya na Mabinti balehe na wanawake Vijana walioko nje ya shule Mkoani Shinyanga wanaonufaika na mradi wa EpiC.
Makabidhiano ya vifaa vilivyotolewa vilivyotolewa na Mradi wa EpiC unaotekelezwa na FHI 360 kwa ajili ya vituo vya afya na Mabinti balehe na wanawake Vijana yakiendelea
Makabidhiano ya vifaa vilivyotolewa vilivyotolewa na Mradi wa EpiC unaotekelezwa na FHI 360 kwa ajili ya vituo vya afya na Mabinti balehe na wanawake Vijana yakiendelea
Sehemu ya vifaa vilivyotolewa vilivyotolewa na Mradi wa EpiC unaotekelezwa na FHI 360 kwa ajili ya vituo vya afya na Mabinti balehe na wanawake Vijana

Wanufaika wa Mradi wa EpiC na wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa
Mnufaika wa mradi wa EpiC Deniza  Paschal akielezea namna alivyonufaika kupitia mradi huo
Mnufaika wa mradi wa EpiC Mhoja Philipo akielezea namna alivyonufaika kupitia mradi huo
Mnufaika wa mradi wa EpiC Mbuke Daudi akielezea namna alivyonufaika kupitia mradi huo
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم