Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu kimetangaza nafasi kwa Wanachama wenye sifa kujitokeza kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo, baada ya Mwenyekiti aliyekuwepo (Juliana Mahongo) kufariki dunia Septemba 15, 2024.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa jana na Katibu wa CCM wilaya hiyo, Ibrahimu Kajanga limetaja sifa za kugombea nafasi hiyo kwamba, awe raia wa Tanzania, awe mwanachama hai wa CCM, aje kusoma na kuandika na pia awe na sifa za ziada zilizotajwa katika katiba ya CCM.
Aliongeza kuwa fomu hizo zitaanza kutolewa kwenye Ofisi ya Katibu wa CCM wilaya ya Bariadi kuanzia tarehe 29 mpaka 31/1/2025 na muda wa kuchukua fomu ni saa 2:00 asubuhi na kujesha saa 10:00 jioni
Mwisho.
Post a Comment