ENG. KUNDO AAGIZA MKANDARASI MRADI WA MAJI TINGATINGA ASIMAMIWE.




Na Mwandishi wetu.


NAIBU Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew, ameagiza wataalam wa  Wakala maji na usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kumsimamia kwa karibu mkandarasi M/S Serengeti Ltd anayetekeleza mradi wa maji wa Tingatinga, uliopo Wilaya ya Longido, Mkoa wa Arusha. 


Mhandisi Kundo ametoa agizo hilo   leo Februari 28, 2025 kwa lengo la kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa ufanisi na kukamilika kwa wakati.


Akizungumza na viongozi wa RUWASA na wakandarasi, Mhandisi Kundo amesema kuwa ni muhimu kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huo ili wananchi wa eneo hilo waweze kupata huduma ya maji kwa wakati.


Pia  amesisitiza kuwa mkandarasi anapaswa kuongeza idadi ya wafanyakazi ili kuhakikisha kazi inaenda kwa haraka na kufikia malengo yaliyowekwa.


Mhandisi Kundo ameeleza kuwa serikali inatoa kipaumbele katika kuhakikisha kuwa miradi ya maji inakamilika kwa wakati ili kuboresha maisha ya wananchi hasa katika maeneo ya vijijini.


Ikumbukwe kuwa, mradi wa maji wa Tingatinga ulianza kujengwa mwezi Machi 2023 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Machi 2025. ambapo hadi sasa, utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 54, na umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.7. 


Mwisho.













Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post