Na COSTANTINE MATHIAS, Chato-Geita.
SERIKALI ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imempatia zawadi ya Trekta mshindi wa uzalishaji wa zao la Pamba katika msimu wa 2023/2024 baada kuzingatia kanuni za kilimo bora cha Pamba.
Mkulima Walwa Selemani, Mkazi wa Kijiji cha Songambele kata ya Ipalamasa wilaya ya Chato Mkoani Geita aliibuka Mshindi kutokana na kuzalisha Pamba kwa tija ambapo alilima akari tatu na kupata kilo 2,700 kwa kila ekari moja.
Akizungumza kwa niaba ya baba yake, Paul Selemani amesema kabla ya kupata elimu ya Kilimo cha Pamba walikuwa wanalima kiholela na kupata mavuno haba, na kuwashauri wakulima waamini kwamba ekari moja inaweza kutoa mavuno mengi kwa kufuata maelekezo ya wataalamu wa kilimo.
"2023 nilipanda kwa kutumia mbolea ya samadi, nikapata kilo 1600 kwa ekari moja, mwaka uliofuata (2024) nilipata mbolea ya Minjingu ya kupandia na kukuzia nikafuata maelekezo ya wataalamu wa kilimo ...kila ekari nilipata kilo 2,775 na kuona Kilimo cha Pamba kinalipa" amesema na kuongeza.
"Naishukuru Bodi ya Pamba kuwa bega kwa bega na wakulima, mwaka huu nimetumia mbolea na vipimo vya 60 kwa 30 natarajia kupata kilo 3,000 mpaka 4,500 kwa ekari moja...kutokana na ushindi wa mwaka jana, Rais Dk. Samia, baba alikabidhiwa Trekta mpya pale Dodoma".
Afisa Kilimo anayeratibu wa zao la Pamba wilaya ya Chato, Ismail Mbaikaize amesema, Walwa Zacharia ni kioo Kwa wakulima wa zao la Pamba sababu analima kwa kufuata kanuni kumi za Pamba ambaye aliibuka Mshindi kutokana na kuvuna kilo 8,000 kwenye ekari tatu sawa na kilo 2,725 na amekuwa sehemu ya hamasa Kwa wakulima wengine wa Pamba.
Mwisho.
إرسال تعليق