MrJazsohanisharma

MAUWASA yatunukiwa Tuzo na EWURA

 

Mkurugenzi Mtendaji wa MAUWASA, Mhandisi Nandi Mathias (kulia) akipokea cheti kutoka kwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dotto Biteko kilichotolewa na EWURA.


Na Samwel Mwanga,Maswa.


MAMLAKA ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Maswa (MAUWASA) iliyoko katika wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu imefanikiwa kushinda tuzo mbili zilizotolewa na Mamlaka ya  Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa mwaka 2023/2024.


Kwa mujibu wa taarifa ya EWURA iliyotolewa Machi 19, 2025 imeonyesha kuwa MAUWASA imeshika nafasi ya tatu katika Mamlaka bora inayotoa huduma bora za maji na usafi wa mazingira katika kundi la pili kati ya Mamlaka nyingine 19 zenye wateja 5,000 hadi 20,000 hapa nchini.


Pia MAUWASA imeshika nafasi ya kwanza kwa Mamlaka iliyofanikiwa kufikia malengo iliyojiwekea katika mpango wake wa biashara (Bussiness Plan).

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt Dotto Biteko alimkabidhi tuzo hizo Mkurugenzi Mtendaji wa Mauwasa, Mhandisi Nandi Mathias jijini Dar Es Salaam katika ukumbi wa Mlimani City.


Naye Mhandisi Nandi Mathias akikabidhi tuzo hizo leo kwa wafanyakazi wa MAUWASA katika ofisi za mamlaka hiyo zilizopo mjini Maswa licha ya kuishukuru EWURA kwa kuwapatia tuzo hizo zilizotokana na ushindanishaji.


Pia amewapongeza wafanyakazi wote wa Mamlaka hiyo na kuhaidi  kuendelea kufanya kazi kwa wekedi,ubunifu na kujituma ili tuendelee kufikia malengo ya taasisi yao hasa kwa kuwahuduma wateja wao kwa kuwapatia huduma bora.


MWISHO.


Mkurugenzi Mtendaji wa Mauwasa,Mhandisi Nandi Mathias(kulia)akipokea cheti kutoka kwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,Dotto Biteko kilichotolewa na EWURA.



Cheti walichotunukiwa MAUWASA na Ewura kwa ajili ya utoaji wa huduma bora.







Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post