RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, leo machi 21, 2025 ameshiriki hafla ya Uapisho wa Rais wa Namibia, Netumbo Nandi-Ndwaitah.
Mara baada ya kuwasilisha, Rais Dk. Samia alipokelewa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako, Windhoek nchini Namibia.
Sherehe hizo pia ziliambatana na maadhimisho ya Miaka 35 ya Uhuru wa nchi hiyo ambapo Rais Samia amealikwa kuwa Mgeni rasmi katika sherehe hizo.
Rais Dk. Samia amempongeza Rais Mteule wa Jamhuri ya Namibia, Netumbo Nandi-Ndwaitah baada ya kuhutubia hafla ya Uapisho iliyofanyika katika Ikulu ya nchi hiyo, Windhoek.
Rais Nandi-Ndwaitah, ni Rais wa kwanza mwanamke kuchaguliwa katika Taifa hilo la Namibia.
Source: Uhuru online.





Post a Comment