RC atangaza Kipindipindu kuisha Simiyu.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kenani Kihongosi.

Na Derick Milton.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kenani Kihongosi ametangaza rasmi leo kuwa ugonjwa wa Kipindupindu ambao uliukumba mkoa huo kwa kipindi kirefu umeisha na hakuna tena mgonjwa au watu wenye dalili za ugonjwa huo.

Akiwa kwenye kikao cha kamati ya ushauri cha Mkoa (RCC) kilichofanyika leo Mjini Bariadi Kihongosi amesema kuwa Wilaya zote ambazo zilikumbwa na ugonjwa sasa ziko shwari na hakuna ugonjwa huo tena.

Amesema kuwa serikali kupitia Wizara ya Afya na wataalumu wa Afya katika mkoa huo wakiwemo wadau wa Afya, walifanya jitihada kubwa kuhakikisha ugonjwa huo unaondoka ndani ya mkoa huo.

“ Leo ninayo taarifa nzuri na njema kwa wananchi wa mkoa wa Simiyu, kuwa ule ugonjwa ambao ulitutesa kwa kipindi fulani sasa umekwisha, mkoa wa Simiyu hakuna kipindupindu tena, tunashukuru sana wale wote ambao walisaidia katika kutokomeza ugonjwa huu,” amesema Kenani.

Ikumbukwe Mlipuko wa Ugonjwa huo umedumu kwa muda mrefu takribani mwaka mmoja, ambapo watu kadhaa walifariki na wengine kupona kutokana na kukubwa na ugonjwa huo.

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم