Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
KAMATI ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Simiyu imeridhishwa na Ujenzi wa miradi mbalimbali ya Maendeleo wilayani Bariadi Mkoani Simiyu katika sekta za Afya, Elimu, Maji na Jengo la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA lililoko Somanda mjini Bariadi.
Aidha, Miradi hiyo imekuwa kielekezo cha Utekelezaji wa Ilani ya CCM ambayo imelenga kuwasogezea wananchi huduma za maendeyna kiuchumi karibu na maeneo yao.
Katibu wa CCM Mkoa huo, Eva Ndegeleki amesema ujenzi wa miradi ya Maendeleo katika wilaya ya Bariadi umetekelezwa kwa kiwango kizuri na kwamba wananchi wanapaswa kumuunga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kumpa kura za kishindo kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi Novemba mwaka huu.
"Miradi mingi imetekelezwa na serikali ya Dk. Samia, kila mahali kuna miradi imetekelezwa, Wajibu wetu ni kumpa kura za kishindo kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi Novemba mwaka huu, tuwape kura za kishindo Madiwani na Wabunge wa CCM watakaoteuliwa ili waendelee kusimamia miradi ya Maendeleo" amesema Katibu huyo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenan Kihongosi amesema kuwa kuna Ushirikiano mkubwa baina ya Chama na serikali ili kuhakikisha miradi ya Maendeleo inatekelezwa kwa kiwango kizuri.
Katika wilaya ya Bariadi, Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Simiyu imekagua Zahanati katika Kijiji cha Nduha iliyojengwa kwa ghamara ya shilingi mil.57.45, Mradi wa Maji Sakwe unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi Bil.1.94.
Pia wamekagua ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari mwamoto inayojengwa la gharama ya shilingi mil. 584.2, Jengo la Malamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) lililoko Somanda lililojengwa kwa shilingi Bil. 9.4, Mradi wa Maji kutoka Ziwa Viktoria wenye thamani ya shilingi Bil. 446 na ujenzi wa Shule ye Sekondari mwakibuga wenye thamani ya shilingi Bil.1.2.
Mwisho.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
Post a Comment