MrJazsohanisharma

KIWANDA CHAKI MASWA KUKUZA UCHUMI NA KUONGEZA AJIRA KWA WANANCHI.

Kiwanda cha Chaki Maswa.


Na COSTANTINE MATHIAS, Maswa.


KUKIMILIKA kwa Ujenzi wa Kiwanda cha Chaki Maswa ambao umegharimu zaidi ya shilingi Bil. 10.1, unatarajia kutoa ajira pamoja na kukuza Uchumi kwa Wananchi katika wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu.


Aidha imeelezwa kuwa Miradi hiyo ya kimkakati itapunguza utegemezi wa mapato kutoka serikali Kuu katika Halmashauri ya wilaya ya Maswa.


Hayo yamebainishwa leo na Afisa Mipango wilaya hiyo, Julia's John wakati akitoa taarifa ya Ujenzi wa Mradi huo mbele ya Kamati ya Saisa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu inayokagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.


Amesema kuwa Kiwanda hicho kitatoa fursa ya ajira kwa vijana ambapo vijana 201 wataajiriwa na pia Halmashauri itapokea gawio la shilingi Mil. 769.6 sawa na asilima 70 ya Pato halisi.


"SUMA JKT alipewa ujenzi kwa shilingi Bil. 4.3 kujenga Kiwanda cha Chaki, Jengo la mtambo wa kuchakata mawe ya gypsum na Dolomite na Jengo la Kiwanda...Mradi umefikia 99, Halmashauri imefanya makubaliano ya Wakala wa Manunuzi ya Serikali (GPSA) ili kusambaza chaki katika shule zote za Serikali" amesema Afisa Mipango.


Ameiomba Wizara ya Elimu kutoa maagizo kwa Maafisa Elimu kote nchini kuhakikisha wananunua chaki za Maswa.


Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Eva Ndegeleki ameiomba Halmashauri hiyo kuhakikisha inawapa kipaumbele Vijana na wananchi wasio na ujuzi ili waweze kufanya kazi na kujipatia kipato.


Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mkoa wa Simiyu (MNEC), Gungu Silanga amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk. Samia imefanya maajabu katika wilaya ya Maswa kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo ujenzi wa Kiwanda cha chaki.


"Kiwanda hiki kilikuwa ndoto, kuna baadhi walitaka kubadilisha mawazo...sasa tumeanza kuona faida ya Mradi huu na kazi yetu tumepita na kuona ujenzi wake, Mradi huu utaleta Mapinduzi makubwa katika Mkoa wa Simiyu, kiuchumi na kutoa ajira kwa vijana." Amesema Gungu.


Mwisho.


Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Simiyu wakipata ufafanuzi juu ya hatua za kutengeneza Chaki.


Levis Charles, ambaye ni Mhandisi Mitambo katika Kiwanda cha Chaki Maswa, akitoa ufafanuzi wa namna ya kuendesha Kiwanda hicho mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Simiyu waliopita kukagua ujenzi wake.


Mitambo ya Kiwanda cha Chaki Maswa.







Levis Charles, ambaye ni Mhandisi Mitambo katika Kiwanda cha Chaki Maswa, akitoa ufafanuzi wa namna ya kuendesha Kiwanda hicho mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Simiyu waliopita kukagua ujenzi wake.


Vijana wakiendelea na kazi katika kiwanda cha Chaki Maswa.


Mawe ya kusaga kwa ajili ya kupata unga wa kutengeneza chaki.

























Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post