Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Andrea Mathew, ameendelea na ziara yake ya kikazi Kata kwa Kata kwa lengo la kuwasilisha utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020–2025 katika kata ya Masewa na kutoa misaada wa vifaa mbalimbali kwa sekta za elimu, maji, michezo na utawala.
Akizungumza kwenye Mkutano maalum wa kuwasilisha Ilani, Mhandisi Kundo amemshukuru Rais Dk. Samia kwa kutoa fedha za miradi ya Maendeleo ili kuboresha upatikanaji wa huduma hususani sekta ya Maji na Mawasiliano kwenye kata hiyo ya pembezoni mwa hifadhi ya Serengeti.
"Tunamshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha za miradi ya Maendeleo, miaka mitano nyuma kata hii haikuwa na Maji, Umeme wala mitandao ya simu...tunamshukuru sana mwezi Oktoba tumpe kura za kishindo" amesema.
Ameongeza kuwa, kutokana na Jimbo la Bariadi kugawanywa, yeye (Mhandisi Kundo) atagombea Ubunge Jimbo la Bariadi vijijini lenye kata 21.
Katika Kata ya Masewa, inayojumuisha vijiji vya Igabanhilo, Senta na Masewa, Mbunge huyo ameendelea kugusa maisha ya wananchi kwa namna ya kipekee Kwa kukabidhi mifuko 60 ya saruji kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba vya Madarasa Shule ya Sekondari Masewa.
Katika hatua nyingine Mbunge huyo ametoa mipira 4 na jezi pea 1 kwa kila Kijiji na kufanya jumla ikiwa mipira 12 na jezi pea tatu huku timu ya kata ikikabidhiwa mipira 3 na jezi pea 1.
Kata hiyo pia imenufaika kwa kupokea pumpu 3 za maji zenye thamani ya shilingi Mil. 10.5, pambu ambazo zimetolewa na Rais Dk. Samia ili kuchochochea jitihada za kuboresha huduma ya maji safi na salama.
"Nimekuwa nikiwahudumia kwa moyo mmoja na leo mnaona matokeo ya kazi yetu. Katika kugawanywa kwa jimbo hili, nimesikiliza maoni yenu na sasa natangaza kuwa nitagombea Ubunge wa Jimbo la Bariadi Vijijini ili tuendelee na kazi ya maendeleo tuliyoianza pamoja," amesema Mhandisi Kundo.
Mwisho.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
















Post a Comment