NGAYIWA ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE KAHAMA MJINI

 

Mbobevu wa duru ya kisiasa wilayani Kahama Mkoani Shinyanga ambaye pia ni Meneja wa Rasilimali Watu wa benki ya CRDB Kanda ya ziwa Ndugu Benjamin Lukubha Ngayiwa amejitokeza tena kuwania nafasi ya Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika uchaguzi wa kura za maoni ndani ya CCM mwaka 2020 Ndugu Ngayiwa alimtikisa vilivyo Mbunge aliyemaliza muda wake ambapo alikuwa mtu wa pili nyuma ya Mh. Jumanne Kishimba kwa tofauti ya kura chache.


Taarifa zilizotufikia zinasema Ndugu. Benjamin Lukubha Ngayiwa ambaye ni msomi na mbobevu wa mambo ya siasa na utawala Juni 28,2025 alifika ofisi za Chama Cha Mapinduzi wilayani Kahama kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba ridhaa ya Wanachama wenzake wa CCM ili wamchague kupeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi katika kinyang'anyiro cha ubunge Jimbo la Kahama Mjini.

Ndugu. Ngayiwa ambaye anapewa nafasi kubwa ya kumpiku Mhe. Kishimba amesema kwamba;  "Muda muafaka ukifika ataweka wazi sababu na nia iliyomsukuma kurudi tena Jimboni kuomba ridhaa ya wananchi".
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post