Shule ya Wasichana Simiyu (Simiyu girls) iliyoko Kijiji Cha Igegu, kata ya Sapiwi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.
Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
SERIKALI ya awamu ya sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imejenga shule mpya ya sekondari ya Wasichana Simiyu kupitia Mradi wa SEQUIP ambayo imekamilika na kuanza kutumika.
Mapokezi ya fedha za mradi huo yalikuwa kwa awamu tatu, ambapo awamu ya kwanza kiasi cha shilingi Bil. 3 zilipokelewa, awamu ya pili shilingi Bil. 1.1 na awamu ya tatu shilingi Mil. 350.
Shule hii imejengwa katika Halmashauri ya wilaya ya Bariadi, kijiji cha Igegu, kata ya Sapiwi ambapo miongoni mwa miundombinu iliyojengwa ni pamoja na Jengo la Utawala, Bwalo, vyumba 12 vya madarasa, mabweni 8, nyumba 2 za walimu, matundu 16 ya vyoo na kichomea taka.
Wananchi wa Mkoa wa Simiyu, viongozi wa serikali, viongozi wa dini, vyama vya siasa na wadau wengine wa Maendeleo, wamemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa takribani Shilingi Bil. 4.45 kwa ajili ya kutekeleza mradi huo mkubwa ambao umekua kielelezo cha maendeleo katika sekta ya Elimu mkoani humo.
Mwisho.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com







Post a Comment