Na Mwandishi wetu, Meatu,
MKUU wa mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha amewaagiza Wakuu wa Wilaya Mkoani humo kufanya operesheni maalum ya kuwasaka na kuwakamata watu wanaochezea mizani janja za kupimia pamba na kuwaibia wakulima na kuwafikisha mara moja katika vyombo vya kisheria.
Macha ameagiza hayo katika ziara yake Wilayani Meatu baada ya kupata taarifa za Wakulima wa zao la Pamba kuibiwa na baadhi ya viongozi wa AMCOS wasio waaminifu.
Meneja wa wakala wa vipimo Mkoani Simiyu, Happy Titi amesema baada ya kufanya ukaguzi walibaini mizani 91 kati ya 235 iliyokaguliwa Wilayani Meatu imechezewa na baadhi ya viongozi wa AMCOS kwa kushirikiana na Wataalamu wa mizani almaarufu vishoka.
Aidha ameeleza kuwa katika Wilaya zote Mkoani Simiyu jumla ya mizani 818 zilikaguliwa ambapo mizani 481 zimebainika kuchezewa na Viongozi wa AMCOS kwa kushirikiana na wataalamu wa mizani wasio rasmi almaarufu vishoka.
Mwisho.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
Post a Comment