![]() |
Katibu wa siasa na uhenezi CCM Mkoa wa Simiyu Lumen Ngunda, akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake leo. (Picha na Derick Milton) |
Jumla ya wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu wapatao 1,024 wameomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi ya udiwani.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Katibu wa siasa na uhenezi CCM Mkoani hapa Lumen Ngunda amesema kuwa kati ya hao 748 wameomba udiwani wa kata na 184 viti maalumu udiwani.
Katika nafasi ya Ubunge Lumeni amesema kuwa mkoa wa Simiyu unayo majimbo 8, ambapo wanachama 101 wanawake wakiwa 12 na wanaume 89 wameomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea ubunge kwenye majimbo hayo.
Hata hivyo katibu huyo wa uhenezi ametolea ufafanuzi
taarifa ambazo zilikuwa zikizagaa katika mitandao ya kijamii kuwa katika jimbo la
Kisesa hakuna mwanachama yeyote ambaye amechukua fomu.
“ Taarifa hizo siyo kweli, kwenye jimbo hilo jumla ya wanachama 14 wamejitokeza kuchukua fomu, wanaume
wakiwa 12 na wanawake wawili,” amesema Lumen.
Post a Comment