MWENGE WA UHURU KUFIKIA MIRADI YA SHILINGI BIL 1.5 BARIADI VIJIJINI.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu, Iddi Ndabhona (kushoto) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bariadi Khalid Mbwana.




Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.


MWENGE wa Uhuru 2025, umepokelewa katika Kijiji cha Mwamoto, Halmashauri ya wilaya ya Bariadi ukitokea Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu. 


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bariadi, Khalid Mbwana amepokea Mwenge huo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Iddi Ndabhona baada ya kukamilisha Mbio zake. 


Ukiwa Halmashauri ya wilaya ya Bariadi, Mwenge huo utakimbizwa kilometa 184 katika Tarafa mbili na kata 8 ambapo utanzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi Bil. 1.5.


Mwisho. 







Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم