MWENGE WA UHURU WATUA ITILIMA, KUZINDUA MIRADI YA SHILINGI BIL. 3.1.

 

Mkuu wa Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, Faudhia Ngatumbura (kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Itilima Anna Gidarya.


Na COSTANTINE MATHIAS, Itilima.


MWENGE wa Uhuru 2025, umeingia katika wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu ukitokea wilaya ya Meatu Mkoani humo, ambapo utakimbizwa kilometa 115.3.


Mkuu wa Wilaya ya Itilima Anna Gidarya ameupokea mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Meatu Faudhia Ngatumbura na umepokelewa katika uwanja wa Shule ya msingi Gambasingu. 


Ukiwa wikayani Itilima, mwenge huo utakagua, Kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi Bil.3.1.


Mwisho.







Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post