MWENGE WAKAGUA KITUO CHA MAFUNZO YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI DUTWA.




Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.


MWENGE wa Uhuru 2025, umekagua Kituo cha Mafunzo ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Uhifadhi wa Mazingira kilichopo Dutwa wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, mradi unaotekelezwa kwa mapato ya ndani kwa gharama ya shilingi Mil. 53.3.


Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, Ismail Ussi ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Bariadi Kwa ujenzi wa kituo hicho ambacho kitawasadia wakulima na wafugaji kupata maarifa.


"Katika mikoa 22 tuliyopita, hatujakutana na jambo la kipekee kama tuliloliona hapa… Hongera sana Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Khalidi Mbwana" amesema Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, Ismail Ali Ussi.


Kituo hicho kitafanya shughuli zifuatazo, Uzalishaji wa mazao (mikunde, nafaka, mafuta, mboga), Ufugaji wa mbuzi, kondoo & ndege, Ufugaji wa samaki aina ya sato na Uzalishaji wa miche 72,253 ya miti ya matunda, kivuli, dawa na mbao


Lengo la Mradi huo ni kuwajengea wakulima na wafugaji uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, na kuhamasisha uhifadhi wa mazingira 


Mwisho.








Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم