Njalu Silanga.
NA COSTANTINE MATHIAS, Itilima.
ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Itilima Mkoani Simiyu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Njalu Daudi Silanga ameshinda kura za maoni kwa kupata kura 8,285 akifuatiwa na Josephine Makongoro aliyepata kura 1822.
Akitangaza Matokeo hayo, Katibu wa CCM wilaya hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi, Joel Makwaia amesema kuwa kura zilizopigwa ni 11, 063, kura halali 10959 na zilizoharibika ni kura 104.
Katibu huyo amewatangaza Wagombea wengine ambao ni Jeremiah Nkulukulu amepata kura 604 na Emmanuel Subi kura 248.
Mwisho.



Post a Comment