“Chukueni tahadhari dhidi majanga ya moto, ajali”

 



 

Na Anita Balingilaki,Simiyu

 

Jamii mkoa Simiyu imetakiwa kuchukua hatua dhidi ya matukio au majanga  ambayo yanaweza kuhatarisha maisha yao, watoto na mali zao.

 

Miongoni mwa matukio au majanga ambayo yametajwa yanaweza kuepukika ikiwa jamii itachukia tahadhari za haraka ni pamoja na ajali za barabarani,  majini, moto na migodini.

 

Hayo yamesemwa leo na kaimu kamanda mkoa Simiyu jeshi la zimamoto na uokoaji  Inspekta Faustin Mtitu ambapo amesema kwa kipindi cha Januari hadi Disemba 2022 jeshi hilo limekabiliana na matukio ya moto 21 na hakuna mtu aliyepoteza maisha.

 

Aidha amesema wamefanya uokoaji kwenye matukio 25 ambayo yanahusisha ajali za barabarani, migodi, mashimo ya vyoo, kusombwa na maji ya mvua, mabwawa na mito na yamesababisha vifo 43.

 

" Matukio hayo yamesebabisha vifo watu 43 wanawake 14 na wanaume 29 kwa upande wa majeruhi walikuwa 114 wanawake 38  na wanaume 76 na matukio yote kwa kipindi hicho hayakihusisha watoto wadogo" amesema inspekta Mtitu.

 

Katika kuhakikisha wananchi wanapata elimu dhidi ya majanga Inspekta Mtitu amesema jeshi hilo kwa kipindi cha Januari hadi Disemba 2022 limeendelea kufanya jitihada za kuzuia majanga ya moto na majanga mengine yasitokee kwenye jamii kwa kufanya ukaguzi wa tahadhari na kinga dhidi ya majanga ya moto kwenye majengo na vyombo vya usafiri na usafirishaji.

 

" Kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita ( 2022) majengo 1,537 na magari 76 yalikaguliwa, maeneo 88 yalipatiwa elimu na wanufaika walikuwa 24,754 wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi kuanzia awali, na  elimu hiyo waliipata kupitia njia ya redio, kwenye  mashule, nyumba za ibada na kwenye mikusanyiko" amesema Inspekta Mtitu na kuongeza kuwa:

 

"Michoro ya majengo 26 ilisomwa na kupitishwa ikiwemo ya nyumba 17 za kuishi, 05 za biashara na vituo vinne vya mafuta,...kwa mwaka uliopita hatukupata matukio yaliyohusisha watoto wadogo ila  mwaka 2020 tarehe 19,Novemba watoto watatu walipoteza maisha kwa kuzama kisimani kwa  nyakati tofauti katika kijiji cha Iwelimo kata ya Mwamanenge wilayani Maswa mkoani hapa" amesema Inspekta Mtitu.

 

 

Annastazia Masanja ni mkazi wa Kidinda Bariadi amesema jeshi la zimamoto limewasaidia kupata elimu mbalimbali ikiwemo ya usalama barabrani na elimu hiyo wameifikisha hadi kwa watoto wao kwa kuwaelekeza namna bora ya kuvuka barabara waendapo shule na wakati wakirudi.

 

 

 

“Kiukweli mimi elimu niliyoipata kutoka jeshi la zimamoto na uokoaji…nakumbuka siku moja  nikiwa mnadani  walifika wakatupa elimu kwa sasa mwanangu mdogo ana miaka saba anajua namna bora ya kuvuka barabara kwa kuzingatia alama zilizopo barabarani” amesema Masanja. 

 

Jisabu Masunga ni mkazi wa mjini Bariadi amesema ni vema sheria ikachukua mkondo wake ili kupunguza / kumaliza majanga hususani ambayo yanaepukika huku Veronika Mwobagulalila akisema bado elimu inatakiwa kwani wapo wanaofanya hivyo pasipo kujua madhara.

 

" Hivi mtu anachimba shimo alafu analiacha hivyo hivyo bila kulifukia unakuta jirani na eneo hilo kuna watoto wadogo sana wengine hata miaka mitano hawajafikia wanacheza karibu na eneo hilo mtu kama huyo bila sheria kuchukua mkondo wake makubwa yanaweza kutokea" amesema Masunga.

 

Miongoni mwa matukio yaliyoteka hisia za wananchi ni  pamoja na ajali za magari ikiwemo ya iliyotokea Januari 11,2022 iliyotokea eneo la Nyamikoma wilayani Busega mkoani hapa iliyosababisha vifo vya watu 15, ajali nyingine iliyotokea Marchi 27,2022 iliyotokea Kidurya wilayani Bariadi iliyohusisha vifo vya watu 7 na tukio la watoto watatu kuzama kwenye visima Novemba 19,2020 wilayani Maswa.

 


Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم