Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange akizungumza na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Mkoani Simiyu, wakati wa ziara yake Wilayani humo. |
Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange akikagua baadhi ya maeneo katika ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Bunda Mkoani Mara. |
Na,
OR-TAMISEMI
Naibu Waziri Ofisi ya
Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange amemsimamisha kazi Kaimu Mhandisi
Halmashauri Wilaya ya Bunda mkoani Mara Timothy Mwajara huku akimtaka
Mkurungenzi wa Halmashauri hiyo Changwa
Mkwazo na Mganga mkuu wa Halmashauri Jamaly Kimamba kujitathimini juu ya utendaji
kazi wao kwa kushindwa kusimamia ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo.
Naibu Waziri amefikia maamuzi hayo leo Januari 13, 2023
wakati akikagua ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo ambapo hakuridhishwa na kasi
ya ujenzi huku thamani ya fedha zilizotumika ikiwa hailingani na kazi
iliyofanyika kwenye ujenzi huo ambao unaendelea ambapo mpaka sasa umeghalimu Bilioni
3.6
Dkt. Dugange amesema
Mhandisi wa Wilaya ya Bunda ana mwaka mmoja tangu ameletwa katika halmashauri
hiyo lakini ameshindwa kusimamia kikamilifu ujenzi wa majengo ya Hospitali hiyo
na kamuagiza Katibu Tawala Mkoa kuleta Mhandisi mwingine atakaweza kusimamia
ujenzi wa hospital hiyo.
Kadhalika, Amemtaka
Mganga mkuu wa Halmashauri kujitafakari utendaji kazi wake ambapo ana miezi
sita tangu ameletwa katika halmashauri hiyo lakini haoneshi ufanisi wa kazi
yake ikiwa ni pamoja na kushindwa kusimamia ujenzi wa Hospital hiyo ya Wilaya
ambao umeanza tangu mwaka 2019.
Dkt. Dugange amesema
wakati akikagua hospitali hiyo ameona kuna vifaa ambavyo vimenunuliwa tangu
mwaka 2019 kama madirisha ya aluminium, milango, vigae na mbao lakini
hayajafungwa katika maeno yake na kupelekea kuharibika na vingine kuibiwa.
Aidha, Dkt. Dugange
amesema tangu mwezi wa tano mwaka 2019 Serikali ilitoa Bilioni 1.8 kujenga
majengo saba ya awali lakini mpaka sasa hayajakamilika kwa sababu Watendaji
waliosimamia ujenzi walifanya ubadhilifu wa fedha na walishindwa
kusimamia.
Ameagiza kupatiwa
majina watumishi wote ambao walihusika katika usimamizi wa ujenzi wa hospitali
hiyo ambao wamehamishiwa maeno mengine ikiwa ni pamoja Waganga wakuu,
Wahandisi, Maafisa manunuzi wa watumishi wengine ili waweze kurudi kujibu
tuhuma na kuchukuliwa hatua sitahiki.
Amemtaka Mkurugenzi na
menejimenti yake kujitafakari juu ya utendaji kazi wao katika usimamizi wa
fedha za miradi ambazo zinaletwa katika halmashauri hiyo lakini hazisimamiwi na
hazitumiki wala kufanya kazi halisi inayopaswa kufanyika.
Pia, Dkt. Dugange
ameagiza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na TAKUKURU kuchunguza thamani
ya fedha iliyotumika kama inaendana na kazi iliyofanyika mpaka sasa na tuhuma
mbalimbali ikiwa ni pamoja na wizi ambao umekuwa ukifanyika mara kwa mara
ili wahusika wote waweze kuchukuliwa hatua sitahiki.
Dkt. Dugange
ameelekeza kuundwa kwa kamati za Ujenzi ambazo zitasimamia ujenzi wa hospitali
hiyo ambapo sasa ujenzi umekuwa ukiendelea bila kuwa na kamati hali
inayopekelea kasi ya utekeleza kudorora na fedha nyingine zifanyiwa ubadhilifu.
إرسال تعليق