Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bariadi mkoani
Simiyu kimezindua sherehe za maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama
hicho kwa kupanda miti katika shule ya Sekondari Guduwi iliyopo katika
Halmashauri ya Mji wa Bariadi ili kulinda uoto wa asili.
Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Katibu Tawala wa wilaya hiyo Nichodemus Shirima amesema Chama Cha Mapinduzi kilizaliwa tarehe 5/2/1977.
Amesema CCM ngazi ya wilaya ya Bariadi inaadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM kwa kupanda miti ili kuenzi juhudi zilizofanywa na viongozi wa Chama ambao walitangulia wakati wa kuasisi CCM.
‘’Tuitunze miti hii ili itutunze, itakuwa ni aibu tunaenzi juhudi za viongozi halafu tunapanda miti inakauka…tutakuwa tunakausha juhudi za Chama, miti ina faidha kadhaa ikiwemo kivuli, hewa nzuri, mbao, mkaa na mvua’’ amesema Shirima.
Katibu Tawala huyo amewataka wananchi kuendelea kupanda miti ya aina mbalimbali ikiwemo ya mbao na matunda katika maeneo yao ili kuendelea kulinda na kutunza uoto wa asili.
Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Bariadi Masanja Salu amesema wamezindua maadhimisha ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM katika kata ya Guduwi na kwamba watahitimisha katika Kasoli kwa kufanya shughuli za kijamii.
Salu amewataka wanaCCM kushikama, kuyasema mazuri yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia ambapo kila kijiji au kata kuna miradi ya maendeleo inayotekelezwa.
Diwani wa Kata ya Guduwi Nhandi Mnyumba amekipongeza Chama cha Mapinduzi kwa kufanya maadhimisho katika kata hiyo huku akiwataka wana chama kuendelea kuiamini serikali iliyoko madarakani.
Edward Robart mkazi wa Guduwi amekipongeza Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kufanya maadhimisho katika kata hiyo huku akisema hajawahi kuona maadhimisho ya CCM yakifanyika katani kwake tangu azaliwa.
MWISHO.
WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari Guduwi wakishiri zoezi la kupanda miti wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaliyofanyika shuleni hapo.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
إرسال تعليق