Mhandisi Kundo awahimiza Vijana matumizi sahihi ya Mitandao.

 

 
 

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia wa Habari, Mhandisi Kundo Mathew, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mkoa wa Simiyu akizungumza kwenye sherehe za Umoja wa Vijana (UVCCM) za kuazimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi zilizofanyika wilaya ya Itilima.

Na COSTANTINE MATHIAS, Itilima.

 

VIJANA wametakiwa kuwa na matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii ili iweze kuwanufaisha badala ya kuitumia kwa mabishano na mijadala isiyokuwa na tija na wakati mwingine kuitumia kwa kutukana na kudhalilisha wengine.

 

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew  wakati akizungumza na Umoja wa vijana wa chama Cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Simiyu wakati wa kusherehekea miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama hicho.

 

Mhandisi Kundo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bariadi, amesema yapo mambo mengi ya kujifunza na yenye tija katika mitandao ya kijamii hivyo ni vyema vijana wakaitumia mitandao hiyo kujifunza na kufanya yaliyo mazuri ili wanufaike kupitia mitandao hiyo.

 

"Mawasiliano ni huduma muhimu kwa kiasi kikubwa ndio maana serikali inafanya jitihada za kuhakikisha inarahisisha huduma za mawasiliano kwa wananchi wake, lakini sasa tumieni vizuri mitandao ya kijamii, itumieni kwa usahihi na kwa tija na si kuitumia vibaya pasipo na faida na pengine kutukana watu." Amesema Mhandisi Kundo.

 

Mbunge wa Jimbo la Itilima Njalu Silanga amesema katika kuhakikisha Vijana wanawezeshwa kiuchumi, katika mwaka wa fedha 2022/2022 wamepewa mkopo wa pikipiki 32, huku wakiwa na mpango wa kutoa zingine 110 ambazo zitakuwa ni sawa na pikipiki tano kila kata.

 

"Tumetoa mikopo ya shilingi milioni 74 kwa wanawake na pikipiki 32 kwa vijana na tuna mpango wa kutoa mkopo wa pikipiki zingine 110 kwa vijana ikiwa na maana kuwa kila kata itapata pikipiki tano hii ni kazi nzuri inayofanywa na chama cha mapinduzi katika kuhakikisha vijana tunawainua kiuchumi . Amesema Njalu.

 

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Itilima Faiza Salim akaipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.

 

"Mheshimiwa Rais ameleta mafanikio makubwa tuna umeme, sasa hivi tunaenda kupata umeme kila kijiji, tunaenda kupata vituo vya afya kila tarafa, tunaenda kuimarisha na kujenga zahati zetu katika vijiji, barabara tumeona zimefunguka kwa kiasi kikubwa, sasa hivi tuna dawa, juzi tumefungua hospitali yetu ya wilaya tumeanza upasuaji vifaa vimeletwa, yapo mengi yaliyofanya tunamsifu sana mheshimiwa Rais kwa kuyaleta katika wilaya ya Itilima. Amesema Faiza Salim.

 

Naye Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Itilima Mhuli Ngeleja ameipongeza serikali ya chama Cha mapinduzi kwa mambo mazuri na makubwa yaliyofanyika yenye kuketa tija kwa wananchi wake.

 

"Tunapoadhimisha miaka 46 ya chama chetu, ni mambo mengi yamefanyika huduma bora za afya katika zahati, vituo vya afya na hospitali zetu, umeme wa uhakika, maji yanapatikana, barabara zimeboreshwa na shule zimejengwa kwa ubora kabisa, imani yetu kwa chama chetu ni kubwa na kitafanya vizuri katika uchaguzi wa mwakani 2024 na hata uchaguzi mkuu 2025." Amesema Ngeleja.

 

MWISHO.

 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post