Na Samwel Mwanga,Maswa.
WAKALA wa Barabara wa
Mjini na Vijijini (TARURA) wilaya ya Maswa mkoani Simiyu wanatarajia kujenga
barabara za kiwango cha lami katika mitaa mitatu katika mjini wa Maswa.
Hayo yameelezwa na
Kaimu Meneja wa TARURA wilaya ya Maswa,Mhandisi Francis Kuya wakati akizungumza
na waandishi wa habari waliotembelea mji wa Maswa kujionea kazi zilizofanywa na
Tarura.
Amesema kwa mwaka wa
fedha 2023/2024 katika kuboresha barabara za mitaa katika mji huo licha ya
kujenga mitaro ya maji ya mvua kwa sasa watajenga barabara za kiwango cha lami
katika mitaa ya Lubala,Kapilima na Ziota.
Mhandisi Kuya amesema
kuwa gharama za ujenzi huo ni kiasi cha Sh Milioni 500 ambazo zinatokana na
Mfuko wa Jimbo la Maswa Mashariki.
"Baada ya
kukamilika kwa ujenzi wa mitaro ya maji katika barabara zetu za kwenye mitaa
sasa tunakwenda kuongeza barabara za kiwango cha lami kupitia fefha za mfuko wa
jimbo,'"
"Mitaa ya
Lubala,Kapilima na Ziota iliyoko mjini Maswa barabara zake sasa zinakwenda
kujengwa kwa kiwango cha lami," amesema.
Amesema kuwa tayari
Mkandarasi wa ujenzi wa barabara hizo zenye urefu wa Kilomita moja amekwisha
kupatikana na tayari ameanza kazi za awali ambazo ni pamoja na kuondoa mabomba
ya maji,nguzo za umeme na kuondoa miamba ya mawe.
Mkuu wa wilaya ya
Maswa,Aswege Kaminyoge ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuweza kuleta
fedha nyingi wilayani humo kupitia Tarura hali ambayo inaifanya wilaya hiyo
kuwa na barabara za kuweza kupitika kwa kioindi chote cha mwaka mzima.
Amesema kuwa miundo
mbinu hiyo ya barabara ni lazima ilindwe kwa gharama zote na kuwaonya watu wote
wanaohujumu miundombinu hiyo kuwa wakibainika watachukuliwa hatua kali za
kisheria.
"Serikali
inatumia pesa nyingi katika miundo mbinu hii ya barabara hivyo ni lazima
tuilinde kwa gharama zote na wale watakaobainika kuhujumu miundombinu hiyo
wakibainika ni lazima tuwachukulie hatua kali za kisheria kila mmoja awe mlinzi
wa mwenzake," amesema.
Tarura katika wilaya
ya Maswa imekuwa ikipokea fedha toka serikali kiasi cha Sh Bilioni 4.226 kwa
mwaka kwa ajili ya kuboresha barabara za wilaya hiyo.
Fedha hizo zinatolewa na serikali kwa mchanganuo wa Sh Bilioni 2 za matengenezo ya barabara zinazotokana na tozo za mafuta,Sh Bilioni moja za Mfuko wa jimbo(jimbo la Maswa Mashariki sh Milioni 500 na Jimbio la Maswa Magharibi Sh Milioni 500)na Sh Bilioni 1.226 zinazotokana na Mfuko wa barabara.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
إرسال تعليق