Rc Nawanda atoa siku 14 ujenzi wa kituo cha afya Mwasengela.

 


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahya Nawanda akisisitiza Jambo, wakati wa ziara yake Wilayani Meatu. (kulia) Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Meatu (kushoto) Mkuu wa Wilaya hiyo


Majengo katika kituo cha Afya Mwasengela.


 

Na Bahati Sonda, Simiyu.

 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahya Nawanda ametoa siku 14 kwa viongozi wa Halmashauri ya Wilaya Meatu Mkoani humo kuhakikisha  Ujenzi wa kituo Cha Afya Mwasengela unakamilika ili wananchi waanze kupata huduma.

 

Dkt Nawanda amesema ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje( OPD) pamoja na maabara kwenye kituo hicho ulianza Januari 17,2022 na ulipaswa kukamilika kwa muda wa miezi 3 suala ambalo limeenda kinyume kwani mpaka sasa ujenzi wake haujakamilika.

 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt Yahaya Nawanda, ametoa agizo hilo mapema leo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi mradi huo, katika siku ya kwanza ya ziara yake Wilayani humo.

 

 

Amesema kuwa serikali ilitoa fedha za kutosha kuhakikisha kituo hicho kinajengwa haraka na wananchi wanaanza kupata huduma, lakini ujenzi haujakamilika na waananchi wanaendelea kuteseka.

 

“ Natoa wiki mbili nitakana ujenzi ukamilike haraka na huduma zianze kutolewa mra moja, ndani ya muda huo nataka nipate taarifa kuwa wananachi wameanza kupata huduma ili wapunge adha ya kuangaika” amesema Dkt. Nawanda.

 

Awali akizungumza wakati mkuu huyo wa mkoa akiwa kwenye mradi huo Diwani wa kata Mlangale Saakumi amemweleza kiongozi huyo kuwa tabia ya wafanyabiashara wa Wilaya hiyo kupandisha gharama za vifaa vya yjenzi ni miongoni mwa sababu iliyochangia kuchelewa Ujenzi huu kukamilika kwa wakati.

 

 

Akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi huo Mganga Mfawidhi Zahanati ya Mwabulutago Edson Nyarugulu amesema kuwa mradi huo umefikia asilimia 86 na hatua nyingine zinazoendelea ni za ukamilishaji wa ujenzi wa mradi huo.

 

Amezitaja changamoto za utekelezaji mradi huo ni pamoja na kutopatikana kwa maji kwa ajili ya ujenzi kutokana na ukame, kuchelewa kuidhinishiwa kwa vifungu vya matumizi na kukosekana kwa fundi sehemu ya kazi kwa ajili ya kumalizia mradi.

 

 

Kwa upande wao wakazi wa Kata ya Mwasengela akiwemo Pendo Mabula wameeleza kuwa wanalazimika kutembea umbali mrefu kwenda kutibiwa Zahanati ya Mwabulutagu na kituo Cha Afya Mwandoya, ambapo kukamilika kwa kituo hicho kutasaidia kuondoa kero hiyo.

 

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt Nawanda ameongoza zoezi la uchangishaji wa pesa kwa ajili ya kuwanunulia sare za shule na mahitaji mengine kwa wanafunzi 8 wa shule ya Sekondari Busangwa walioripoti wakiwa na sare za shule ya Msingi kufuatia wazazi wa wao kukosa pesa za kuwanunulia.

 

         Mwisho.

 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post