Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahya Nawanda akisisitiza Jambo, wakati wa ziara yake Wilayani Meatu. (kulia) Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Meatu (kushoto) Mkuu wa Wilaya hiyo |
Majengo katika kituo cha Afya Mwasengela. |
Na Bahati Sonda,
Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Dkt. Yahya Nawanda ametoa siku 14 kwa viongozi wa Halmashauri ya Wilaya
Meatu Mkoani humo kuhakikisha Ujenzi wa kituo Cha Afya Mwasengela
unakamilika ili wananchi waanze kupata huduma.
Dkt Nawanda amesema ujenzi
wa jengo la wagonjwa wa nje( OPD) pamoja na maabara kwenye kituo hicho ulianza
Januari 17,2022 na ulipaswa kukamilika kwa muda wa miezi 3 suala ambalo
limeenda kinyume kwani mpaka sasa ujenzi wake haujakamilika.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Dkt Yahaya Nawanda, ametoa agizo hilo mapema leo wakati akikagua maendeleo ya
ujenzi mradi huo, katika siku ya kwanza ya ziara yake Wilayani humo.
Amesema kuwa serikali
ilitoa fedha za kutosha kuhakikisha kituo hicho kinajengwa haraka na wananchi
wanaanza kupata huduma, lakini ujenzi haujakamilika na waananchi wanaendelea
kuteseka.
“ Natoa wiki mbili
nitakana ujenzi ukamilike haraka na huduma zianze kutolewa mra moja, ndani ya
muda huo nataka nipate taarifa kuwa wananachi wameanza kupata huduma ili
wapunge adha ya kuangaika” amesema Dkt. Nawanda.
Awali akizungumza
wakati mkuu huyo wa mkoa akiwa kwenye mradi huo Diwani wa kata Mlangale Saakumi
amemweleza kiongozi huyo kuwa tabia ya wafanyabiashara wa Wilaya hiyo
kupandisha gharama za vifaa vya yjenzi ni miongoni mwa sababu iliyochangia
kuchelewa Ujenzi huu kukamilika kwa wakati.
Akisoma taarifa ya
ujenzi wa mradi huo Mganga Mfawidhi Zahanati ya Mwabulutago Edson Nyarugulu amesema
kuwa mradi huo umefikia asilimia 86 na hatua nyingine zinazoendelea ni za
ukamilishaji wa ujenzi wa mradi huo.
Amezitaja changamoto
za utekelezaji mradi huo ni pamoja na kutopatikana kwa maji kwa ajili ya ujenzi
kutokana na ukame, kuchelewa kuidhinishiwa kwa vifungu vya matumizi na
kukosekana kwa fundi sehemu ya kazi kwa ajili ya kumalizia mradi.
Kwa upande wao wakazi
wa Kata ya Mwasengela akiwemo Pendo Mabula wameeleza kuwa wanalazimika kutembea
umbali mrefu kwenda kutibiwa Zahanati ya Mwabulutagu na kituo Cha Afya
Mwandoya, ambapo kukamilika kwa kituo hicho kutasaidia kuondoa kero hiyo.
Katika hatua nyingine
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt Nawanda ameongoza zoezi la uchangishaji wa pesa kwa
ajili ya kuwanunulia sare za shule na mahitaji mengine kwa wanafunzi 8 wa shule
ya Sekondari Busangwa walioripoti wakiwa na sare za shule ya Msingi kufuatia
wazazi wa wao kukosa pesa za kuwanunulia.
Mwisho.
إرسال تعليق