Kaimu Mkuu wa Takukuru wilaya ya Maswa,Alpha Malisa akitambulisha program ya Takukuru-Rafiki kwa wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Wilaya hiyo(hawapo pichani)katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo |
Na Samwel Mwanga,Maswa.
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU)
katika Wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu imetambulisha Program mpya iitwayo
TAKUKURU-Rafiki ili kuongeza ushiriki wa kila mwananchi na wadau katika
kukabili tatizo la rushwa katika utoaji wa huduma kwa jamii na utekelezaji wa
miradi ya maendeleo.
Kaimu Mkuu wa Takukuru wilaya ya Maswa,Alpha Malisa
akitambulisha program hiyo kwa wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC)
katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo amesema kuwa itatekelezwa katika ngazi ya Kata kwa ajili ya kutambua kero zilizopo kwenye utoaji
na upokeaji wa huduma za kijamii kama vile Elimu au Afya pamoja na mchakato wa
kutekeleza miradi ya maendeleo kama Ujenzi wa miundombiniu ya Maji.
Amesema kuwa Kwa kufanya hivyo watatambua kero ambazo zikiachwa
pasipo kutatuliwa au kupatiwa ufumbuzi zinaweza kusababisha kutokea Kwa vitendo
vya Rushwa.
"Hii program itaanzia kwenye ngazi ya Kata na diwani wa
Kata ndiye atakuwa Mwenyekiti wa vikao hivyo na huko tutatambua kero zilizoo
kwenye jami hasa katika kutekeleza hii miradi ya maendeleo inayopeleka na
serikali huko Kwa Wananchi,"
"Pia program hii inaakisi maana ya neno rafiki kwa kubeba
dhana ya kuwa karibu na kushirikiana na Wananchi na wadau kuondoa kero katika
jamii,"amesema.
Amesema kuwa moja ya faida ya program hiyo itachangia kukuza
Ustawi wa utawala bora kwa kuzuia vitendo vya rushwa visitokee katika utoaji wa
huduma kwa Umma au katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
"Hii itachangia kuboresha huduma zinazolewa na Umma na
wadau wengine pia kuokoa fedha kwa kujengwa na kutekelwzwa miradi bora,endelevu
na inayokidhi thamani ya fedha iliyotumika.
Aidha Malisa ametoa wito kwa Wananchi kushirikiana na Takukuru
kuzuia vitendo vya rushwa visitokee katika njia ya utoaji wa huduma kwa Umma na
utekelezaji wa miradi ya maendeleo hivyo wananchi wasikae penbeni katika
kutekeleza program hiyo Ili kwa pamoja kuijenga Tanzania.
Mkuu wa wilaya ya Maswa,Aswege Kaminyoge amesema kuwa iwapo
program hiyo ikitekelezwa itapunguza au kuondoa vitendo vya rushwa katika jamii
hivyo ameiomba jamii kuipokea na kulifanyia kazi.
"Hii program ikitekelezwa kama tulivyoelezwa na Kaimu Mkuu
wa Takukuru wilaya ya Maswa nina imani itapunguza au kuondoa vitendo vya rushwa
katika jamii hasa katika miradi ya maendeleo inayopelekwa na serikali kwa
Wananchi.
Mwisho
إرسال تعليق