Baadhi ya wakulima katika Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, wakiwa wamebaba Vinyunyizi (Pampu) kwa ajili ya kunyunyizia dawa za kuua wadudu, mara baada ya kugawiwa na Bodi ya Pamba nchini. |
Mkaguzi wa Pamba Wilaya ya Itilima kutoka Bodi ya Pamba Said Itaso, ikamkabidhi mkulima Kinyunyizi (Pampu) kwa ajili kwenda kuunza kupulia dawa kwenye shamba lake. |
Mkaguzi wa Pamba Wilaya ya Itilima kutoka Bodi ya Pamba Said Itaso, ikamkabidhi mkulima Kinyunyizi (Pampu) kwa ajili kwenda kuunza kupulia dawa kwenye shamba lake. |
|
Na Derick Milton, Simiyu.
Wakulima wa zao la Pamba katika Wilaya ya Itilima
Mkoani Simiyu, wameishukuru serikali kupitia Bodi ya Pamba nchini kwa kuja na
utaratibu mpya wa ugawaji wa vinyunyizi (Pampu) pamoja na viuatilifu mapema.
Mbali na hilo wamepongeza zoezi la ugawaji wa
pembejeo hizo kufanyika mapema kabla ya wadudu hawajaanza kushambulia, hasa
wakiwemo funza ambao muda wa kuanza kushambulia zao hilo umekaribia.
Wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
zoezi la ugawaji wa Pampu awamu ya tatu kumalizika, wakulima hao wamesema kuwa
wamefuraishwa zaidi kupewa pampu za kutosha.
Paulina Boniphace mmoja wa wakulima amesema kuwa
changamoto kubwa ambayo ilikuwa inawakabili wakulima ni suala la upatikanaji wa
pampu, kwani kwenye kijiji unaweza kukuta pampu zipo mbili au tatu.
Amesema wamefurahishwa na hatua hii ya bodi ya
pamba ya kuwaletea pampu za kutosha, ambapo kwa mwaka huu hakutakuwa na
changamoto hiyo tena kwani wakulima wengi akiwemo yeye wamepata.
“ Hapa kwenye kijiji utakuta pampu zipo hata 20,
tulikuwa tunateseka sana hasa wale wakulima wenye hekari nyingi, tunashukuru
sana Bodi ya pamba, lakini tunashukuru pia hizi pampu zimekuja mapema pamoja na
dawa” amesema Paulina.
Naye Joseph George mkulima amesema kuwa hatua ya
Bodi ya pamba kuleta viuatilifu mapema ni jambo kubwa sana, kwani muda wa funza
kuanza kushambulia pamba umekaribia.
“ Hatujawahi kupewa dawa mapema hizi, lakini awamu
hii tunaona wamejipanga na wakulima tumelima sana, wadudu wamekaribia, lakini
tayari dawa tumepatiwa, uko nyuma mpaka tupige kelele, wadudu wanashambulia
shamba zima ndiyo wanaleta dawa” amesema George.
Mkaguzi wa Pamba Wilaya ya Itilima kutoka Bodi ya
Pamba Said Itaso, amesema kuwa mpaka sasa wamegawa vinyunyizi awamu tatu,
ambapo katika awamu ya kwanza walitoa Pampu 218, awamu ya pili 1,500, na
awamu ya tatu 782.
Amesema kuwa katika msimu huu Bodi ya pamba
imejipanga kwa nguvu kubwa, kuhakikisha hakuna pamba ambayo itaharibiwa na
wadudu hasa viwavijeshi, huku akiwataka wakulima kwenda kutumia vifaa hivyo
ipasavyo.
“ Zoezi hili tumelifanya kwa wakulima wakubwa
kwanza wale wenye kuanzia hekari tano, tukiwapatia hawa ni rahisi kuwaazima
wale wenye hekari chache, uko nyuma wengi walikuwa wanaangaika kupata pampu
lakini leo tumewapa wote” Amesema Itaso.
Mkaguzi huyo ameongeza kuwa katika Wilaya ya
Itilima mpaka sasa pamba haijaanza kushambulia na wadudu, ambapo ameeleza
wakulima wote tayari wamepatiwa dawa za kutosha za kuua wadudu hao.
MWISHO.
Post a Comment