DK. Nawanda awasisitiza Watendaji Kusoma Mapato na Matumizi ya Vijiji.

MKUU wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwamapalala kwenye Mkutano wa hadhara.

MKUU wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda amewataka watendaji wa Vijiji na kata kuhakikisha wanasoma mapato na matumizi katika maeneo yao kutokana na fedha za maendeleo zinazoletwa na serikali pamoja na michango ya wananchi.

 

Dk. Nawanda ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mwamapalala na Kidula wilayani Itilima mkaoni humo wakati akikagua shughuli za maendeleo.

 

Amesema suala la kusoma mapato na matumizi katika mkoa wa Simiyu ni jambo la lazima ili wananchi waweze kujua michango ya serikali, wananchi pamoja na wadau wa maendeleo.

 

‘’niwatake watendaji wa vijiji na kata, suala la kusoma mapato na matumizi ni la lazima katika mkoa wangu..hata kama hakuna watu, someni mapato na matumizi hata kama kuna watu wawili, someni mapato na matumizi’’ amesema.

 

Katika hatua nyingine Dk. Nawanda amewasisitiza wananchi kupeleka watoto shule ili wakasome na kupata elimu kutokana na serikali kujenga madarasa kwa gharama kubwa.

 

Alimwagiza mtendaji wa Kijiji cha Kidula kuhakikisha anawarejesha wanafunzi wanne ambao hawajaripoti shule mpaka sasa huku akisisitiza kuwa wanafunzi wanatakiwa kuripoti shuleni hata kama hawana sarem madaftari na viatu.

 

MWISHO.


MKUU wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda akimpa maelekezo Mkuu wa Wilaya ya Itilima Faidha Salim kuhusu kuwasimamia watendaji wa vijiji kusoma mapato na matumizi.

 


 Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa Hadhara kijiji cha Mwamapalala wilayani Itilima.

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم