Na
Mwandishi wetu, Simiyu.
Matukio ya mauji ya watu mbalimbali hasa watoto,
wazee, na wanawake yakitajwa kusababishwa na imani za kishirikiana, migogoro ya
kifamilia katika Mkoa wa Simiyu yanadaiwa kurejea tena.
Miaka mitano nyuma matukio haya yalikomeshwa kwa
kiwango kikubwa. Sasa yanatajwa kuanza kurejea upya kutokana na taarifa za kila
siku kuonyesha lazima kuwepo kwa tukio mtu kuuawa.
Kabla ya kukomeshwa, Mkoa wa Simiyu ulisifika kwa
matukio hayo, ambapo waganga wa tiba asili walitajwa kuwa kichocheo kikubwa cha
uwepo wa matukio hayo kwa wingi.
Kuanzia wiki iliyopita viongozi wa Mkoa huo kwa
nyakati tofauti tofauti likiwemo Jeshi la Polisi, wamezumgumzia kurejea kwa matukio hayo.
RC.
Mkuu wa Mkoa Dkt. Yahya Nawanda akiwa kwenye hafla
ya kukabidhi zawadi Askari waliofanya vizuri mwaka 2012, iliyofanyika Februari
04, 2023 (jumamosi ya wiki iliyopita) alizumgumzia matukio hayo.
Kwa mujibu wa Dkt. Nawanda kwenye Hafla hiyo
ambayo alikuwa mgeni rasmi, alisema kuwa kila siku amekuwa akipewa taarifa na
Kamanda wa Polisi Mkoani humo uwepo wa matukio mauaji.
Dkt. Nawanda amesema kuwa matukio ya mtu kuuawa
kwa imani za kishirikina au migogoro ya kifamilia, yameanza kuongezeka kwani
kila siku lazima kuwepo kwa tukio.
Anasema kuwa matukio yanayosababishwa na imani za
kishirikina ndiyo yamekuwa mengi, yakifuatiwa na migogoro ya kifamilia, pamoja na
ukataji wa mapanga, ambapo wazee, wanawake na watoto ndiyo waanga.
“ Kila siku RPC akinipigia simu utasikia
anakwambia leo kuna mtu mmoja ameuawa, siku nyingine akisema hakuna tukio
unamshukuru Mungu, lakini haya matukio sasa yameongezeka, yamekuwa mengi,”
anasema Dkt. Nawanda….
“ Hizi tabia tumezitoa wapi sisi wasukuma, mbona
sisi siyo watu wa hivi, hizi tabia mbona zilipotea, sasa zinatoka wapi?”
anasema Dkt. Nawanda.
Mkuu huyo wa Mkoa anawataka wagaga wa tiba asili
kuanzisha kampeini ya kupita vita kurejea kwa matukio hayo, huku akilitaka
jeshi la kupambana na hali hiyo.
DC.
Siyo tu Mkuu wa Mkoa ambaye amezungumzia kuanza
kurejea kwa matukio ya mauji mkoani hapa.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Simon Simalenga akizungumza
na waandishi wa Habari jana, amesema kuwa ndani ya wiki moja jumla ya watu
watano wameuawa, wakiwemo watoto, wazee na wanawake.
“ Uko nyuma haya mauji yalikomeshwa kabisa, lakini
tumeona yanataka kuanza kurudi, ndani ya wiki moja watu watano wameuawa, wapo
watoto, wazee na wanawake, na yote yanahusishwa na imani za kishirikina ikiwemo
migogoro ya kifamilia,” Amesema Simalenga.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa akiwa kama Mkuu
wa Wilaya hiyo, atahakikisha matukio hayo yanakomeshwa huku akitumia msemo kuwa
“ Afe kipa, afe Beki, lazima mauji Bariadi yakomeshwe,” amesema Simalenga.
RPC.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa Blasius Chatanda
kwenye hafla ya kutoa zawadi kwa Askari, anakiri matukio ya mauji kuanza
kuongeza ambapo anasema wameanza kupambana nayo.
Chatanda anasema wanawashirikisha wadau mbalimbali
wakiwemo waganga tiba asili katika kupambana na matukio hayo ili kuweza
kukomeshwa kabisa.
MWISHO.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
إرسال تعليق