Hospitali ya wilaya ya Bariadi kutoa Huduma za dharura, Upasuaji mwezi Machi, 2023.

Baadhi ya mashine kwenye jengo la Dharura katika Hospitali ya Wilaya ya Bariadi eneo la Dutwa kwa ajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa.

 

  Jengo la Dharura kwenye Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi (Dutwa) ambalo limekamilika kwa ajili ya kutoa huduma, jengo hilo limegharimu shilingi milioni 300.


Mganga Mfawidhi wa Halmashauri ya wilaya ya Bariadi Dk, Flavian Jacobo akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) kifaa maalumu (test lung) katika mashine inayotumika kumsaidia mgonjwa kupumua.


Baadhi ya mashine au vifaa tiba katika jengo la Dharura katika hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Bariadi.
 

Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.

HOSPITALI ya Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu iliyopo eneo la Dutwa, imekamilisha ujenzi wa Jengo la dharura, upasuaji pamoja na wodi mbili kwa ajili ya kutolea huduma za matibabu kwa wagonjwa.

Ujenzi huo ambao umegharimu jumla ya shilingi bilioni 1.1 umewezesha kupatikana majengo ya kisasa na vifaa tiba vilivyotolewa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

 

Akizungumza mara baada ya kufanya ukaguzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Khalid Mbwana aliipongeza serikali kwa kuwaletea vifaa tiba pamoja na fedha a ujenzi wa majengo ya kisasa.

 

Amesema kwa mwaka wa fedha 2022/2023 serikali ilileta kiasi cha shilingi bilioni 1.1, ambapo milioni 800 zimetumika kujenga wodi mbili, jengo la upasuaji pamoja na jengo la kuhifadhia maiti.

 

‘’Kulikuwa na kiasi cha shilingi milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la dharura (EMD) ambalo limekamilika tayari kwa kutoa huduma…tarehe 1/3/2023 tunategemea rasmi kuanza kutoa huduma ya upasuaji kwa akina mama wajawazito baada ya kukamilika kwa jengo la upasuaji’’ amesema Mbwana.

 

Ameeleza kuwa siku hiyohiyo watazindua huduma za dharura ambapo vifaa tiba ikiwemo vitanda 6, mashine za kusaidia kupumua (ventilators) 8 na mashine za kuangalia maendeleo ya mgonjwa vimeshafungwa katika jengo hilo.

 

Ameongeza kuwa watahakikisha wanatoa huduma bora pia wanasimamia na kulinda vifaa hivyo ambavyo vina thamani kubwa kwa ajili ya kulinda uhai wa wananchi.

 

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk. Flavian Jacob ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuwapatia vifaa tiba vya kisasa vilivyogharimu shilingi milioni 400 vitawasaidia kutoa huduma bora na kuokoa maisha ya wagonjwa.

 

‘’Tumepokea sunction machine, infution pump 6, syringe pum 2, defebrigate 2, vitanda viwili vya kubebea wagonjwa na vitanda sita vya kisasa kwa ajili ya kubebea wagonjwa…Rais ametusaidia tumepata SG machine 1, portable Ultra sound 1, kompyuta ya kisasa inayomsaidia muuguzi kuangali wagonjwa sita kwa wakati mmoja’’ amesema.

 

Ameongeza kuwa kutokana na kompyuta hiyo, muuguzi anaweza kujua hali ya maendeleo ya kila dalili za mgonjwa zinapobadilika ili aweze kuchukua hatua ya kuwahudumia kwa uharaka zaidi.

 

Bahame Kalugula, mkazi wa kijiji cha Sengerema ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuwapatia vifaa tiba ambavyo vitasaidia kuoka maisha ya wagonjwa ambao walikuwa wakiifuata huduma hiyo hospitali ya Bugando.

 

Naye Juma Gitili mkazi wa kata ya Dutwa amesema wagonjwa watapata huduma bora na hakuna mgonjwa atakayehangaika bali watapatiwa tiba katika hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Bariadi iliyopo Dutwa.

MWISHO.

 

Baadhi ya mashine kwenye jengo la Dharura katika Hospitali ya Wilaya ya Bariadi eneo la Dutwa kwa ajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa.
 

 

 Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Bariadi Dk. Flavian Jacobo akiwaonyesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) vitanda viwili vinavyoendeshwa kwa mfumo wa Umeme (Remote control) katika jengo la dharura ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wagonjwa.
 
 

Wodi ya wakina mama katika Hospitali ya wilaya ya Bariadi eneo la Dutwa.
 

Wodi ya wakina mama katika Hospitali ya Wilaya ya Bariadi, Dutwa.
 

Jengo la Dharura Hospitali ya wilaya ya Bariadi iliyoko Dutwa.


Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم