Mkuu wa Kitengo cha M-Mama kutoka Kampuni ya mitandao Vodacom Rahma Bajum akizungumza na wadau wa Afya mkoani Simiyu (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa M-mama Mkoani humo.
Na Derick Milton, Bariadi.
Mfumo huo ambao
kitaifa ulizinduliwa mwaka 2022 na Rais Dkt Samia Suruhu ambapo lengo lake ni
kuhakikisha hakuna kifo cha mama mjamzito na mtoto mchanga kinatokea.
Ukiwa umenafanya kazi katika zaidi ya Mikoa sita mpaka sasa leo
mfumo huo umezinduliwa rasmi mkoani Simiyu, ambapo wadau wa Afya wameeleza kuwa
uwepo wa teknologia hiyo itsaidia sana kuboresha huduma za rufaa na za dharura.
Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Yahya Nawanda amesema kuwa Mkoa wa Simiyu
bado unakabiliwa na uwepo wa vifo vya mama wajawazito, ambapo ameeleza kuletwa
kwa mfumo huo utasaidia katika mapambano ya vifo hivyo.
“ Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2022 vifo vitokanavyo na uzazi
29 vimetokea, tatizo hili kwa mkoa bado ni kubwa, ni lazima kufikia vifo
sifuri, na ili kufikia lengo hili watalaamu, wadau wote lazima twende
kutekeleza mfumo huu kwa ufasaha,” amesema Dkt. Nawanda.
Dkt. Nawanda amesema kuwa Rais Dkt Samia amedhamilia kuhakikisha
hakuna kifo hata kimoja kinatokea kwa sababu za uzazi, na ndiyo maana
ameendelea kuboresha huduma mbalimbali za Afya ikiwemo kuleta mfumo wa M-Mama.
Daktari kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Majeda Kihulya
amesema kuwa huduma za dharura kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya
zimekuwepo kwa muda mrefu lakini bado zimeendelea kukubwa na changamoto
mbalimbali.
Amesema kuwa Baadhi ya Changamoto ni miumbombinu ya Barabara,
mwitikio mdogo wa wananchi kuhudhulia kliniki, lakini pia wanawake wengine
kuendelea kujifungulia majumbani, ambapo mfumo huo umelenga kutatua changamoto
hizo.
Dkt. Kihulya amesema katika utekelezaji wa Mfumo huo, unaanzia
ngazi za vituo vya Afya, ambapo usafiri wa serikali (Ambluance) na ule usafiri
wa watu binafsi utatumika katika kuhakikisha huduma inatolewa haraka kwa mteja.
Mkuu wa Kitengo cha M-Mama kutoka Kampuni ya mitandao Vodacom
ambao ni washirika katika mfumo huo Rahma Bajum amesema kuwa kupitia mfumo huo
kiongozi yeyote wa Afya anaweza kuangalia jinsi mfumo unavyofanya kazi muda wowote
akiwa ofisini.
“ Kuna wakati unaweza kukuta watu wameomba huduma, lakini hakuna
ambaye ameshughulikia yale maombi, na kiongozi wa Afya wakati huo akaingia
kwenye mfumo, akakutana na hiyo hali anaweza kusadia na huduma ikatolewa kwa
haraka” ameeleza Bajum.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu Fauzia Hamidu amesema kuwa kwenye eneo
la vyombo vya moto vya watu binafsi vinavyotakiwa kuhusuka kusafirisha mgonjwa,
ni vyema hata maeneo ya vijijini yakaangaliwa kwa umuhimu zaidi.
“ Watalaamu wametwambia kuwa yatatumika magari ya wagonjwa (Ambulance)
na Pikipi za mataili matatu (bajaji) kwenye Wilaya zetu ambazo maeneo yake ni
ya vijiji huo usafiri hautumiki sana, zinatumika pikipiki za mataili mawili,
tunaomba huo mfumo uangalie zaidi na jambo hilo,” amesema Mkuu huyo wa Wilaya.
MWISHO.
Post a Comment