Wakazi 6,223 kunufaika na Mradi wa Maji Mwashegeshi,Maswa.

Wananchi wa Kijiji Cha Mwashegeshi wilaya ya Maswa waliohudhuria katika hafla ya Mauwasa ya kumkabidhi mkandarasi,Bal BUILDERS LTM kutekeleza Mradi wa Maji katika Kijiji hicho.

 

Baadhi ya Viongozi wa Serikali wa Kijiji Cha Mwashegeshi wilaya ya Maswa wakiwa na Wafanyakaziv wa Mauwasa wakati wa hafla ya kumkabidhi Mkandarasi  BAL BUILDERS LTM eneo la Mradi wa Maji ya bomba katika Kijiji hicho.


Na Samwel Mwanga,Maswa.


MAMLAKA ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Maswa (Mauwasa) iliyoko katika wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu inatekeleza Mradi wa Maji safi ya Bomba katika Kijiji Cha Mwashegeshi.


Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mauwasa aliyewakilishwa na Leonard Mnyeti wakati wa hafla ya kumtambulisha Mkandarasi BAL BUILDERS LTM ambaye ndiye atatekeleza mradi huo,kwa wananchi wa kijiji hicho.


Akitoa taarifa kwa wananchi juu ya Mradi huo Mnyeti alisema kuwa utagharimu kiasi cha sh milioni 500.7 na Mkandarasi huyo atafanya kazi chini ya Usimamizi wa Mamlaka hiyo.


"Mradi huu wa maji utagharimu kiasi cha sh 530,752,361.50 na huyu mkandarasi ambaye tunamtambulisha kwenu atafanya kazi chini ya uangalizi wetu sisi Mauwasa na si vinginevyo,"alisema.


Alisema kuwa kijiji hicho licha ya kupakana na bwawa la New Sola ambacho ndicho chanzo kikuu cha maji katika mji wa Maswa na vijiji 11 lakini walikuwa si wanafaika wa maji hayo.


Alisema mtandao wa maji katika mradi huo utakapokamilika utakuwa wa kilomita 14.3 na utakamilika ndani ya kipindi Cha miezi tisa.


"Tunategemea ndani ya miezi tisa mradi utakuwa umekamilika na mkandarasi atatukabidhi na mtaanza kupata maji safi na salama na mtandao wetu wa Maji utakuwa wa kilomita 14.3 hivyo niwaombe wananchi mpatieni mkandarasi ushirikiano Ili mradi umalizike kwa wakati,"alisema.


Aidha aliomba uongozi wa Kijiji hicho kuhakikisha kuwa wale baadhi ya wafugaji wanaoingiza mifugo yao kwenye bwawa hilo wanawazuia kwani wakiachiwa watasababisha kukauka Kwa bwawa hilo kwa kuingiza kiasi kikubwa cha tope.


Diwani wa Kata ya Nguliguli,Peter Mlyandengu Mathias ameipongeza serikali kwa kutoa fedha ambazo zitatekeleza mradi huo ambapo ametoa rai kwa wananchi kulinda miundombinu itakayowekwa ya maji ili iweze kudumu kwa muda mrefu.


Alisema kuwa kijiji hicho lilikuwa na shida ya maji safi na salama licha ya kuwa walinzi wa bwawa la New Sola hivyo Mradi huo utakapokamilika Ile adha ya kusafiri umbali mrefu kutafuta Maji watautumia kufanya shughuli za uzalishaji mali.


Pia alisema  kuwa wako tayari kumpatia ushirikiano mkandarasi huyo huku akisisitiza wananchi wa kijiji hicho hasa vijana kupatiwa kazi katika mradi huo ambazo ziko ndani ya uwezo wao.


MWISHO.

 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post