RC Simiyu ahimiza Wazazi kuchangia chakula mashuleni.

MKUU wa Mkoa wa simiyu Dk. Yahaya Nawanda (mwenye miwani kushoto) akikabidhi kilo 25 za sukari kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mwakimisha Celestine Mapesa (kulia) ili wanafunzi waweze kupatiwa uji shuleni.

 

Na COSTANTINE MATHIAS, Itilima.

 

MKUU wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda amewataa Wazazi na Walezi kujenga tabia ya kuchangia chakula mashuleni ili wanafunzi waweze kupata chakula ili waongeza muda wa vipindi mashuleni.

 

Ameyasema hayo mara baada ya kukagua ujenzi wa shule ya msingi Mwakimisha iliyopo kijiji cha Ikungulipu wilayani Itilima  iliyojengwa na shirika la World Vision Tanzania ili kuwapunguzia wanafunzi adha ya kutembea mwendo mrefu.

 

Amesema katika shule hiyo, serikali imeleta kiasi cha shilingi milioni 25 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ili kuunga mkono juhudi za wafadhili pamoja na wananchi.

 

‘’Nimeona nguvu za wafadhili na wananchi, madarasa yamejengwa mazuri sana…vijana tuwe na umoja wa kujitolea, serikali haiwezi kujenga kila kitu, lakini pia tuchangie chakula mashuleni ili watoto waweze kupata uji’’ amesema.

 

Akiwa shuleni hapo, Dk. Nawanda amechangia kilo 25 za sukari ili wanafunzi wa darasa la awali waweze kupatiwa uji, pia alichangia fedha kwa ajili ya kununulia sare, viatu na madaftari kwa wanafunzi sita ambao aliwakuta shuleni hapo wamevaa nguo za nyumbani.

 

Awali akisoma taarifa, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Celestine Mapesa amesema shule hiyo ilianzishwa tarehe 5.8.2021 ikiwa na wanafunzi darasa la awali na la kwanza.

 

Amesema hadi sana shule hiyo ina darasa la awali, la kwanza hadi la nne ambao walihamia kutoka shule ya Ikungulipu A na B na kwamba walipokea shilingi mil. 25 kutoka serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa.

 

‘’Mradi wa vyumba viwili vya madarasa ulilenga kuondoa upungufu wa vyumba vya madarasa, kupunguza mlundikano wa wanafunzi darasani kwa kuzingatia sera ya elimu ya wanafunzi 69 kwa darasa moja’’ amesema Mapesa.

 

Joshua Mabula mkazi wa Kijiji cha Mwakimisha amesema shule hiyo ilianzishwa ili kuwapunguzia wanafunzi adha ya kutembea umbali mrefu wa kilometa 10 kila siku.

 

MWISHO.

MKUU wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda akiwa amembeba mmoja wa wananfunzi wa darasa la awali shule ya msingi Mwakimisha iliyoko kijiji cha Ikungulipu wilayani Itilima.

 

 MKUU wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda akizungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Mwakimisha iliyoko kijiji cha Ikungulipu wilayani Itilima.


Wanafunzi wa darasa la awali shule ya msingi Mwakimisha iliyopo kijiji cha Ikungulipu wilayani Itilima.

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post