Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, Simon Simalenga |
Na Derick Milton, Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, Simon
Simalenga ametoa muda wa miezi miwili kwa watu wote waliokopeshwa na
Halmashauri ya Mji wa Bariadi kupitia asilimia 10 kurejesha kiasi cha zaidi ya
Shilingi Milioni 185 ambacho hakijarejeshwa.
Simalenga ametoa maagizo hayo leo, wakati wa hafla
ya kutoa mikopo kwa vikundi 56 vya wajasliamali kutoka Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, ambapo kati ya vikundi hivyo 46 ni vipya.
Amesema kuwa vikundi vinavyodaiwa pesa hizo,
vilipewa mikopo kwa muda mrefu, lakini mpaka sasa wameshindwa kurejesha, ambapo
ameeleza hatokuwa na mzaha kwenye suala la urejeshaji wa pesa hizo.
Amesema kuwa Rais Dkt Samia Suruhu Hassan amekuwa
akitoa fedha hizo kupitia Halmashauri kwa lengo la kuwakomboa wanawake, vijana,
na watu wenye ulemavu, ambapo amewataka watu wanaonufaika na mikopo hiyo
kukumbuka kurejesha kwa wakati ili na wengine waweze kupata.
Amesema kuwa fedha hizo zinazotolewa siyo sadaka,
ambapo ameeleza baadhi ya watu wamekuwa na nia hovu juu ya mikopo hiyo kwa
kuichukua kisha kukimbia wakidhani hawatafuatiliwa.
“ Kuna sehemu nilikwenda nikakuta wanadaiwa zadi
ya Bilioni moja, huo moto tuliowapelekea hawawezi kusahau mpaka sasa,
walizirejesha zote, na hizi Milioni 185 ni pesa ndogo sana, watazirejesha tu,”
amesema Simalenga...
“ Natoa muda wa miezi miwili, pesa zote ziwe
zimerejeshwa haraka, sitakuwa na mzaha kwenye hili, na niwaambie hata mwende
sehemu yeyote lazima hizi pesa mzirejeshe, ndani ya muda huo ziwe zimerejeshwa,”
ameeleza Simalenga.
Baadhi ya wanufaika wa Mikopo hiyo wameishukuru
serikali kupitia kwa Dkt. Samia Suruhu kwa kuwapatia mikopo hiyo ambayo imekuwa
ikiwawezesha kufanya biashara zao na wamepata maendeleo.
“ Huu ni mkopo wa tatu tunatapa, kikundi chetu
kimekuwa kikipata mkopo ya asilimia 10 na tumekuwa tukirejesha kwa wakati,
mikopo hii imetusaidia sana, leo hii tunamiliki Kampuni kutokana na mkopo wa
Halmashauri,” amesema Mariamu Magese.
إرسال تعليق