Watoto wawili wa Familia ya Tandula Ngasa, katika Kijiji Cha Mwakiloba Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, wamepoteza maisha na wengine saba kunusurika kifo baada ya kudaiwa kula chakula chenye sumu.
Akiwa kwenye mkutano wa Jukwa la tatu la Ushirika Mkoa wa
Simiyu ambapo alikuwa mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Yahya Nawanda amesema
kuwa watoto walipoteza maisha mara baada ya kula chakula hicho.
Dkt. Nawanda amesema kuwa watoto wengine saba ambao
walinusurika, wamekimbizwa katika Hospitali ya rufaa ya Bugando Mkoani Mwanza
kwa ajili ya kupata matibabu zaidi.
Nawanda amesema kuwa Tandula Ngasa ambaye ni Baba wa Familia
alimaka Asubuhi na kwenda alipulizia sumu ya kuua wadudu kwenye shamba la
Pamba, ambapo jioni mke wake naye alikwenda kwenye shamba hilo hilo bila ya
kujua na kuchuma mboga za majani kwa ajili ya chakula.
“ Mama baada ya kuchuma mboga hizo na kwenda kupika bila ya
kujua kama mme wake Asubuhi alipulizia Sumu ya kuua wadudu, walikula mboga hizo
ndipo watoto wakaanza kuumwa” amesema Dkt. Nawanda…
“ Watoto wawili walipoteza maisha (hakuwataja majina) lakini
wengine saba walikimbizwa hospitali Bugando Mkoani Mwanza, na wanaendelea na
matibabu,”
Juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi mkoa Blasius Chatanda
kwa ajili ya kuelezea undani wa tukio hilo zimegonga mwamba, licha ya
kupatikana lakini Kamanda hiyo alisema kuwa yupo nje ya Ofisi kikazi hivyo
hawezi kuliongelea mpaka arudi kutoka safari.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

Post a Comment