Simalenga: Waandishi wa Habari zingatieni weledi.

 

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Simon Simalenga, akizungumza wakati wa maazimisho siku ya uhuru wa vyombo vya habari Mkoani humo, Mkuu huyo wa Wilaya alimwakilisha Mkuu wa Mkoa Dkt. Yahya Nawanda ambaye alikuwa mgeni rasmi.

Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu Faidha Salim akizungumza wakati wa maazimisho ya siku ya uhuru wa Vyombo vya habari Mkoani humo.

Mwandishi wa Habari wa Shirika la Habari la DW kanda ya Ziwa, Alex Mchomvu akitoa mada ya Umuhimu wa siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari wakati wa maazimisho hayo Mkoani Simiyu, yaliyoandaliwa na Klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu (SMPC) kwa kushirikiana na Umoja wa Klabu za waandishi wa Habari Tanzania (UTPC)

Katibu Msaidizi wa Klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu (SMPC) Derick Milton.

Mwenyekiti wa Kamati ya Miradi SMPC Mwandishi wa Habari Sitta Tuma.


Klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu (SMPC) kwa kushirikiana na Umoja wa Klabu za waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) jana imeazimishia siku ya uhuru wa Vyombo vya Habari Mkoani humo, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Yahya Nawanda.

Hafla hiyo ilihudhuliwa na wadau mbalimbali wa Habari mkoani humo, zikiwemo taasisi za kiserikali, wafanyabishara, vyama vya siasa, viongozi wa Dini, waandishi wa Habari pamoja na wafugaji kutoka maeneo mbalimbali mkoani humo.

Akizungumza wakati wa maazimisho hayo, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa ambaye alikuwa mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Simon Simalenga aliwataka waandishi wa Habari kuzingatia weledi katika kutoa taarifa zao.

Simalenga alisema kuwa serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa waandishi wa Habari hasa wa Mkoa wa Simiyu, ikiwemo kutatua Changamoto ya upatikanaji wa Bima za Afya ili kuweza kufanya kazi kwa amani.

Awali akizungumza Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu, Frank Kasamwa, aliwashukuru wadau mbalimbali wa Habari Mkoani humo ambavyo wamekuwa wakitoa ushirikiano kwa wanahabari pamoja na Klabu hiyo.

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post