Takukuru: Walinzi soko kuu Bariadi wanajilipa wenyewe.

 



Taasisi ya kuzuia na kupamba na rushwa Mkoa wa Simiyu (TAKUKURU) imesema kuwa mfumo wa uendeshaji wa soko kuu la Bariadi hauko sahihi kwenye eneo la ulinzi pamoja na mazingira ya ufanyaji Biashara.


Kwenye taarifa yake kwa waandishi wa Habari iliyotolewa leo na Naibu mkuu wa taasisi hiyo Aron Misanga, amesema kuwa wamebaini kuwa walinzi kwenye soko hilo wamekuwa wakijilipa wao wenyewe kinyume na utaratibu.


Amesema kuwa mbali na hilo walinzi waliopo kwenye soko hilo, wengi hawana ujuzi wala taaluma yeyote inayohusiana na ulinzi, huku kwenye malipo wakihusika kukusanya wao pesa kutoka kwa wafanyabishara na kujilipa wenyewe.


“ Lile soko lipo chini ya Halmashauri, walinzi waliopo wamekuwa wakikusanya pesa kwa wafanyabishara kisha kujilipa wenyewe, pesa wanazokusanya hazijulikani ni kiasi gani na wanajilipa kiasi gani,”


Tumewashauri Halmashauri kubadilisha mfumo huo, kwani kwa taasisi ya serikali haukubaliki na wanatakiwa kuboresha mazingira ya ufanyaji wa biashara kwa wafanyabishara pamoja na wananchi wanaopata huduma kwenye soko hilo.


Aidha taasisi hiyo imesema kuwa eneo la njia za kupita kwa wateja katika soko hilo zimekuwa ndogo sana, huku wakibainisha kuwa soko hilo halina maji huku mfumo wa kuzoa taka ukiwa na changamoto.


MWISHO.



Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم