Afisa utumishi, PSSF wachezea mfumo na kumstaafisha Mtumishi kabla ya muda Simiyu. alilipwa Milioni 72, akapokea Milioni 2 tu.

 


Katika hali isiyokuwa ya kawaida Ofisa Utumishi mmoja ambaye alihudumu katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu kwa kushirikiana na Afisa kutoka mfuko wa hifadhi ya jamii PSSF wanaida kuchezea mfumo na kusataafisha watumishi wa serikali kabla ya muda.

Licha ya Maafisa hao kitendo hicho, mtumishi huyo alilipwa Milioni 72 kama mafao yake baada ya kustaafishwa, jambo la kinyama na la kuumiza zaidi ulifanywa mchezo na taasisi moja ya kifedha iliyokuwa inamdai mtumishi huyo ambapo alikatwa kiasi Cha Sh. Milioni 70, na kumbakizia kiasi cha Sh. Milioni 2.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya Nawanda leo kwenye kikao cha Baraza maalumu la Madiwani Halmashauri ya Mji wa Bariadi la kujadili hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG), ndiye ameeleza jambo hilo.


Dkt. Yahaya Nawanda amesema kuwa kitendo hicho ni cha kinyama, ambapo ameagiza Maafisa hao kutafutwa popote walipo hata kama wamehamishwa na amehaidi kupambana nalo hadi hatua kali zichukuliwe dhidi yao.

Amesema kuwa Maafisa hao walikuwa wanachezea mfumo wa utumishi, ambapo mtumishi anashtukia anapigiwa simu kuwa anastaafu jambo ambalo siyo kweli, lengo likiwa ni kutaka kujipatia fedha kwa njia haramu.


“Huyu Afisa utumishi na afisa wa PSSF baada ya kufanikiwa kumstaafisha, huyu mtumishi kuna kampuni moja ya kifedha ilikuwa inamdai, wakala njama, akaingiziwa penshioni yake Milioni 72, walichomfanyia ni kitu cha kinyama, wakamtaka Milioni 70 akabaki na Milioni mbili tu” amesema Nawanda….


“ Nimeagiza uchunguzi uanze mara moja, tunakwenda kuunda tume tuchunguze jambo hili, lakini huyu Afisa Utumishi na Afisa wa PSSF watafutwe popote walipo waje hapa watueleze kwani nini walifanya jambo hili,” ameeleza Nawanda.


MWISHO.


Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم