CCM yataka wanachama kuchangamkia kadi za Kielektroniki.

KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Masanja Salu akiungumza na wanachama wa CCM kata ya Ihusi na kutolea ufafanuzi namna ya upatikanaji wa kadi za kielektroniki.
 
 
Katibu wa CCM wilaya ya Bariadi Masanja Salu akiteta jambo la Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo Juliana Mahongo kwenye kikao cha ndani kilichofanyika Mwaumatondo shule ya Msingi, kulia ni Mwenyekiti wa kata hiyo pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Bariadi Tinana Masanja.



Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.

 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu kimewataka wanachama wa CCM kuchangamkia fursa ya kupata kadi mpya za kielekroniki ili waweze kutambulika, kuongeza wanachama na kuendelea uhai wa Chama.

 

Hayo yamesemwa  na Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo Juliana Mahongo kwenye ziara ya kukagua Uhai wa Chama, Hali ya Kisiasa, pamoja na maandalizi ya uchaguzi wa serikali kwa ngazi ya vijiji na vitongoji 2024 katika vijiji vya Ihusi na Mwaumatondo.

 

Mwenyekiti huyo amesema Chama Cha Mapinduzi kinaendelea kusajili wanachama wake nchi nzima kwa mfumo wa kadi ngumu (Kielektroniki) ili waweze kutambulika kwenye mfumo wa Chama.

 

‘’CCM imeendelea kutekeleza Ilani ya maendeleo kwa kuwaletea wananchi miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye sekta za afya, Maji, Umeme, Barabara na huduma za afya…tunao wajibu wa kupita na kukagua utekelezaji wake pamoja na kupata wanachama wapya’’ amesema.

 

Mwenyekiti huyo amewataka viongozi wa CCM kuendelea kuelimisha wana CCM ili walipe ada na waweze kuwa wanachama hai ili kuendeleza uhai wa Chama Cha Mapinduzi na pia kuongeza wanachama zaidi.

 

Alisema Uhai wa Chama Cha Mapinduzi ni pamoja na Uhai wa Jumuiya zake ambazo ni Umoja wa Wanawake (UWT), Umoja wa Vijana (UVCCM) na Jumuiya ya Wazazi ambazo zinatakiwa kufanya mikutano na wanachama wake ili kubaini changamoto zinazowakabili na kuzitatua.

 

Kwa upande wake Katibu wa CCM wilaya ya Bariadi Masanja Salu amewataka wana CCM kutumia mfumo wa simu kulipa ada za uanachama kwa kutumia makampuni ya Tigo, airtel, Vodacom na TTCL ili kuendelea kuwa wanachama hai.

 

Amesema wanachama wengi wa CCM hawajalipa ada, hivyo wanatakiwa kulipa ada ili kuingizwa katika mfumo wa wanachama hai kwa kupata kadi za kielekitroniki ambazo zinatawasaidia kutambulika uanachama wao.

 

Amewakata wanachama ambao wameshasajiliwa, kufika ofisi za CCM wilaya ya Bariadi kwa ajili ya kupatiwa kadi hizo pamoja na kulipa ada za uanachama ili kuendeleza uhai wa Chama na Jumuiya zake.

 

MWISHO.

 





 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم