Ahukumiwa kuchapwa viboko 8 kwa kosa la kubaka.

Mahakama ya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu.


Na COSTANTINE MATHIAS, Itilima.

 

MAHAKAMA ya Hakimu, wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, imemuhukumu Boniphace Abel (18), msukuma , mkulima na mkazi wa kijiji cha Nyashimba wilaya ya Magu mkoani mwanza adhabu ya kuchapwa viboko vinane kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 17 na kumsababishia majereha.

 

Sambamba na adhabu hiyo, Mahakama pia imetaka mshitakiwa huyo kumlipa mhanga kiasi cha shilingi laki tatu (300,000) kama fidia kutokana na kitendo alichomfanyia.

 

Akitoa hukumu hiyo, hakimu wa mahakama hiyo Robert Kaanwa aliamuru mshitakiwa kupimwa kwanza afya yake na daktari kama anaweza kuhimili adhabu hiyo ya viboko.

 

Awali kabla ya hukumu hiyo, Mwendesha Mashtaka kutoka ofisi ya mashitaka ya Wilaya ya Itilima, Mkaguzi Masaidizi wa polisi Jaston Mhule aliiambia mahakama hiyo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 130 (1) (2)e na 131(2) vya sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

 

Mhule aliileza mahakama hiyo kuwa Mshitakiwa akiwa katika msibwa wa babu yake, mnamo tarehe 10/7/2023 katika kijiji cha Mahembe ndani ya wilaya ya Itilima alimbaka mhanga mwenye umri wa miaka 17 na kumsababishia maumivu.

 

MWISHO.

 

Mahakama ya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu.
 
 
 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم