Na COSTANTINE MATHIAS, Itilima.
Taasisi iisiyokuwa ya kiserikali ya Junior And Child Care Foundation (JACCAFO) imeanza kukutana na viongozi wa ngazi za kata sita wilayani Itilima Mkoani Simiyu kwa ajili ya kujitambulisha, kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa vijana, wasichana, wanawake na watoto.
Aidha, viongozi wa JACCAFO ngazi ya kata wametakiwa kuibua changamoto ikiwemo ukatili za vijana, wanawake, wazee na watoto zinazojitokeza vijijini ili serikali iweze kuzishughuliki.
Akizungumza wakati wa utambulisho, Mwenyekiti wa JACCAFO wilaya ya Itilima Samson Lubimbi amesema taasisi hiyo haifungamani na upande wowote wa kisiasa au kidini na kwamba wanafanya kazi hizo za kizalendo kwa kujitolea.
Amesema taasisi hiyo inaibua changamoto katika jamii hasa vijijini ili serikali na wadau waweze kuisaidia jamii kutatua changamoto ikiwemo watoto wanaokosa elimu kwa kukosa mahitaji maalumu hasa sare za shule na wenye ulemavu kufichwa majumbani.
‘’JACCAFO ni sauti ya waiso na sauti (Voice of the Voiceless), taasisi yetu imesajiliwa kwa namba 00NGO/R/2689 na makao makuu yako Simiyu…tunafanya kazi kizalendo ili kuibua changamoto katika jamii hasa vijijini’’ amesema Mwenyekiti huyo.
Katibu wa JACCAFO wilaya ya Itilima Salunga John amewataka vijana kujitolewa kwa moyo wa uzalendo kuibua changamoto za kijamii katika maeneo yao ili taasisi hiyo iweze kuwafikia na kuzifikisha serikalini.
Amesema watoto wengi wanakosa haki ya msingi kupata elimu kutokana na kukosa watu wa kufikisha sauti zao serikali, hivyo taasisi hiyo imelenga kupaza sauti ya kwa watu wasiokuwa na sauti.
Katika wilaya ya Itilima, JACCAFO imekutana na viongozi kutoka kata za Bumera, Mwaswale, Mwamtani, Ikindilo Nkuyu na Sagata na kwamba zoezi hilo ni endelevu ili kuhakikisha kata zote 22 za wilaya ya Itilima zinafikiwa.
MWISHO.
إرسال تعليق