Serikali yaanza Ujenzi wa VETA Meatu, UWT yapongeza.

MAKAMU Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Taifa Zainabu Shomari (wa pili kushoto) akipata ufafanuzi kutoka kwa mafundi wanaotekeleza mradi wa ujenzi wa chuo cha VETA wilayani Meatu, kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohamed.
 

 

Na COSTANTINE MATHIAS, Meatu.

 

SERIKALI ya awamu ya sita Chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu imeanza Ujenzi wa Chuo cha Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA) katika kijiji cha Bulyashi kata ya Mwamishali wilayani Meatu Mkoani Simiyu kitakachogharimu kiasi cha shilingi Bil. 1.4.

 

Aidha, kukamilika kwa chuo hicho kitaongeza fursa ya ajira na vijana kupata elimu na ujuzi wa ufundi stadi ili kuweza kujiajiri na kupungua changamoto ya ukosefu wa ajira ambao unawakabili vijana kwa sasa.

 

Mthibiti Mkuu Ubora wa Shule wilaya ya Meatu ambaye ni Msimamizi wa Mradi Faustine Lagwen amesema ujenzi wa chuo na mafunzo ya ufundi stadi unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itagharimu shilingi Bil. 1.4.

 

Ameeleza kuwa miundombinu itakayojengwa kwa awamu ya kwanza ni karakana ya mapishi, ushonaji, useremala, uashi, ufundi bomba na umeme, jengo la utawala, jengo la TEHAMA, mifumo ya maji safi na salama, nyumba ya mkuu wa chuo, jengoa la umeme na ofisi ya mlinzi.

 

Amefafanua kuwa mradi huo umewanufaisha makundi mbalimbali ya watu kwa kujipatia kipato ikiwemo kushiriki shughuli za vibarua, ulinzi uzaji wa bidhaa, mbogamboga na vyakula.

 

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo, Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Taifa Zainabu Shomari amesema Umoja huo umeridhishwa ya ujenzi wa Mradi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) wilayani Meatu Mkoani Simiyu unaotelekezwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia kwa gharama ya shilingi Bil. 1.4.

 

Amesema ujenzi huo utaongeza ujuzi na ufundi stadi kwa vijana na watu wazima ambao watapata utaalamu zaidi ili kupata ajira kwenye miradi ya serikali na kupunguza tatizo la ajira nchini jambo ambalo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

 

Ameleeza kuwa ujenzi wa Vyuo vya ufundi stadi nchini ni utekelezaji wa ilani ya CCM kwa kila wilaya ambapo aliwapongeza viongozi wa serikali kwa kusimamia mradi huo ambao umetoa ajira na kuongeza vipato kwa vijana na akinamama lishe.

 

‘’kukamilika kwa chuo hiki, vijana wengi watapata ajira baada ya kujiendeleza katika fani mbalimbali…miradi mingi ya serikali inahitaji wataalamu wenye vyeti, kupitia chuo hiki wataweza kupata ajira’’ amesema Makamu huyo.

 

Amewataka wakandarasi wanaotekeleza mradi huo kuhakikisha wanakamilisha kwa wakati ili ifikapo mwezi Januari 2024 vijana waweze kuanza kupata ujuzi wa ufundi stadi.

 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohamed amempongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kutoa fedha na kuelekeza ujenzi wa VETA kila wilaya.

 

Amewataka wasimamizi na mafundi ujenzi kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa chuo hicho unakamilika kwa wakati ili vijana walioko mtaani waweze kupata elimu ya ufundi stadi.

 

‘’Tutaendelea kuikagua miradi hii ili ijengwe kwa kiwango na ubora na tutahakikisha fedha hizi hazipotei ili kutekeleza ahadi na malengo ya Rais Samia aliyokusudia kuyafanya kwa ajili ya wananchi…nasi muda wote tuko hapa Chama kama macho yake kusimamia’’ amesema Shemsa.

 

MWISHO.

 

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Taifa Zainabu Shomari (wa pili kulia) akitembelea eneo la ujenzi wa chuo cha VETA wilayani Meatu, kulia ni Mbunge wa Vijana mkoa wa Simiyu Lucy Sabu, wa tatu kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Shemsa Mohamed pamoja na Diwani wa kata ya Mwamishali Christopher Ndamo.


Viongozi wakisikiliza taarifa ya ujenzi wa Mradi wa Chuo cha Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA) wilayani Meatu mkoani Simiyu.

 


Mdhibiti Ubora Mkuu wa Shule wilayani Meatu ambaye pia ni Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa Chuo cha VETA, Faustine Lagwen (wa kwanza kulia) akisoma taarifa ya ujenzi wa Chuo hicho mbele ya Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Taifa Zainabu ShomariMakamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Taifa Zainabu Shomari, alipotembelea pamoja na viongozi wengine kwa ajili ya ukaguzi hii leo.


Picha ya pamoja.
 
 
 
 
 
 

 

 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post