Wanawake wapongeza ujenzi wa Wodi za akina mama Vijiji.

MKUU wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda (mwenye skafu katikati) pamoja na viongozi mbalimbali wakikata utepe kuzindua wodi ya wakinamama zahanati ya Mwamlapa iliyoko Kata ya Kasoli Bariadi Mkoani Simiyu.


na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.

 

WANAWAKE wakazi wa Vijiji vya Mwamlapa na Nduha, Kata ya Kasoli wilayani Bariadi Mkoani Simiyu wameipongeza serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa wodi za kujifungulia akinamama vijijini.

 

Wamesema wodi hizo zimekuwa mkombozi kwa wanawake na watoto jambo ambalo linapunguza vifo visivyokuwa vya lazima vilivyokuwa vikitokea kutokana na ukosefu wa huduma na miundombinu ya afya.

 

Maria John Kachwele mkazi wa Mwamlapa amesema wakati hakuna wodi hiyo, wakina mama walikuwa wanatembea kilometa 30 kwa ajili ya kupata huduma ya kujifungua, ambapo aliipongeza kampuni hiyo kwa kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu.

 

Naye Sung’hwa Njile, mkazi wa Nduha ameipongeza serikali kwa kuendelea kuimarisha huduma za afya vijijini kwa kujenga miundombinu ili kurahisisha utoaji wa huduma jambo ambalo limepunguza vifo vya akinamama na watoto.

 

‘’tunaona kila mahali kuna zahanati, vituo vya afya…lakini pia serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wanaendelea kuimarisha miundombinu ikiwemo majengo, vifaatiba na watoa huduma, tunaamini hali hii itarahisisha upatikanaji wa huduma’’ alisema.

 

Awali akizungumza kabla ya kukabidhi jengo hilo, Meneja wa Alliance Ginnery Boaz Ogolla amesema huko nyuma wananchi wa kijiji cha Mwamlapa na Nduha walichangishana fedha ili kukamilisha ujenzi huo lakini hawakuweza kufanikiwa.

 

Anasema, kujengwa kwa wodi hiyo ni ushindi kwa wananchi na kwamba jengo hilo limekamilika kwa asilimia 100 kutokana na ushirikiano baina ya viongozi wa serikali, wadau wa maendeleo na wananchi.

 

Amefafanua kuwa, lengo lilikuwa ni kujenga wodi ya wakinamama kwa muda wa miezi mitatu, lakini kutokana na mchangowa nguvu kazi ya wananchi, jengo hilo limefanikiwa kukamilika ndani ya miezi miwili na limegharimu kiasi cha shilingi mil. 79.7.

 

‘’Ujenzi utaeleta ufanisi wa kupunguza adha ya wakinamama kukosa mahali ya kujifungulia, kuboresha huduma za afya kwa akina mama wanaokwenda kujifungua…tukilitunza vizuri tutalinda afya ya mama na mtoto na pia kuna fursa ya ajira kwa wauguzi na wahudumu wengine’’ amesema Ogolla.

 

Ameongeza kuwa jengo hilo limegharimu shilingi milioni 79 likijumuisha vitanda 6, njia ya kutembelea wagonjwa na uzio huku kiwanda hicho kikijenga kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali ya CQuestCapital na For Women Foundation.

 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda anawataka wananchi kulitunza jengo hilo ili wodi ya akinamama iweze kukaa kwa muda mrefu na wananchi waone faida yake.

 
Anasema jengo hilo lina vitanda saba kwa ajili ya kujifungulia, huku akimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi (Khalid Mbwana) kuhakikisha anaongeza vitanza sita ili kurahisisha utoaji wa huduma.


MWISHO.


Wananchi wakazi wa Vijiji vya Mwamlapa na Nduha wakiwa kwenye hafla ya kukabidhia wodi ya wakinamama iliyojengwa na Kampuni ya Alliance Ginnery kwa kushirikiana na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ya CQuestCapital na For Women Foundation.


Jengo la Wodi ya wakinama Kijiji cha Mwamlapa Kata ya Kasoli wilayani Bariadi lililojengwa kwa gharama ya shilingi mil. 79 likiwa na vitanda 6, uzio na njia ya kutembelea wagonjwa (walk way).
 


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda (wa pili kulia) akikagua moja ya vitanda vya kujifunguliwa kwenye wodi ya wakinamama kijiji cha Mwamlapa, wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bariadi Juliana Mahongo pamoja na Boaz Ogolla (wa tatu kushoto).
 


Kitanda cha kujifungulia wakinamama kwenye wodi ya wanawake kijiji cha Mwamalapa.
 


Kitanda cha kulaza wagonjwa ndai ya wodi ya wanawake katika zanahati ya kijiji cha Mwamlapa.




 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم