Dk. Charles Msira ambaye ni Kaimu Daktari wa
Wanyama wilaya ya Maswa (mwenye koti jeupe) akipatia Mbwa chanjo ya kichaa cha
Mbwa kwenye viwanja vya Madeco.
Na Samwel Mwanga, Maswa.
WANANCHI wa wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu wametakiwa kuwapeleka Mbwa wanaowafunga ili waweze kupata chanjo ikiwa ni sehemu ya mkakati wa wilaya hiyo kudhibiti ugonjwa wa kichaa cha Mbwa.
Hayo yameelezwa leo Septemba 28, mwaka huu na Mkuu wa Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi katika halmashauri ya Wilaya ya Maswa,Robert Urassa wakati wa Maadhimisho ya siku ya Kichaa Cha Mbwa dumiani yaliyofanyika katika Uwanja wa Madeco mjini Maswa.
Amesema kuwa wilaya hiyo imepanga kutoa chanjo kwa wanyama ambao ni Mbwa na Paka ili kudhibiti ugonjwa huo ambao ni hatari kwa maisha ya binadamu iwapo utampata.
Amesema kuwa lengo hilo litakamikika iwapo wananchi watajitokeza kuchanja wanyama hao wenye dalili na wasio na dalili ya kichaa cha Mbwa ili kuzuia madhara yatokanayo na ugonjwa huo.
"Wilaya ya Maswa tumejipanga kuthibiti ugonjwa huu wa kichaa cha Mbwa hivyo malengo yetu ni kuhakikisha tunachanja Mbwa wote pia na Paka mlionao kwenye nyumba zenu hivyo nitoe msisitizo kwa wananchi kuleta wanyama hao ili waweze kupatiwa chanjo," amesema na kuongeza.
"Wale Mbwa ambao wanazurula hovyo mitaani ambao hawana uthibiti tutafanya utaratibu kwa kuwaondoa kwa kuwaua na kama una Mbwa wako ni vizuri ukamtunza vizuri nyumba usimuache azurule hovyo hovyo mtaani na hakikisha walao anapata chanjo walao mara mojja kwa mwaka mmoja,"
Amesema kuwa chanjo hiyo inayolewa Bure na serikali hivyo wananchi hawana budi kuleta wanyama hao ili waweze kupatiwa chanjo hiyo na Mbwa ambaye ameupata hata kuwa na madhara hata kama atamng'ata mtu.
"Hii chanjo inayolewa Bure na Serikali yetu inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu na Mbwa akishapata chanjo hii hata akimng'ata mtu hakutakuwa na madhara yoyote ambaye mtu atayapata hivyo niwaombe tumieni fursa hii kuwachanja wanyama hao,"amesema.
Amesema kuwa wilaya hiyo pia imechukua hatua mbalimbali ili kudhibiti ugonjwa huo na hadi sasa hatua mbalimbali zimeshachukuliwa ikiwemo amri ya zuio la Mbwa kuzurura,utoaji wa Elimu kwa wananchi namba ya kujikinga ili wasipate maambukizi ya ugonjwa huo sambamba na kuwaondoa Mbwa wa mitaani wasio na wamiliki ambao ndiyo wamekuwa chanzo kikubwa cha kusambaa kwa ugonjwa na kuhatarisha usalama wa Afya ya Jamii.
Naye Kaimu Daktari wa Mifugo wilaya ya Maswa,Dk Charles Msira amesema kuwa katika kipindi chaa Mwezi Januari hadi Septemba mwaka huu kumekuwepo na Mbwa wenye dalili ya kichaa cha Mbwa na kushambulia baadhi ya wananchi ambapo ugonjwa huo umeripotiwa katika Kata za Nguliguli,Isabga,Sukuma,Buchambi, na Lalago .
Kata nyingine ambazo ugonjwa huo umeripotiwa ni pamoja na Binza,Nyalikungu ,Shanwa na Sola ambapo vifo vilivyoripotiwa ni watu watatu.
"Kwa binadamu virusi vya kichaa Cha mbwa huweza kuingia mwilini kwa njia ya kung'atwa au kulambwa jeraha na mnyama aliyearhirika na kusambaa kupitia Mfuko wa mishipa ya fahamu na uti wa mgongo hadi kwenye ubongo.
"Sisi wataalamu wa mifugo katika wilaya ya Maswa tunaungana na dunia kwa ujumla kutumia siku hii muhimu katika kuhamasisha Wananchi wa wilaya ya Maswa kuchanja Mbwa wao wote kwani chanjo ni njia pekee inayoaminika kitabibu katika kudhibiti kuenea kwa magonjwa mbalimbali dumiani kutokana inamuwezesha kiumbe kijitengenezea kinga yake ya mwili dhidi ya vimelea vya ugonjwa husika"amesema
Baadhi ya wananchi walioleta Mbwa wao kupata chanjo George Nyagawa Mkazi wa Uwanja wa ndege na Elia Masanja Mkazi wa Sola wilayani hapa wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti waliiomba serikali kulifanyia zoezi hili kuwa endelevu na kuwafuata Wananchi katika maeneo yao wanayoshi hasa maeneo ya vijijini ili wanyama hao wapate chanjo.
Maadhimisho ya Siku ya Kichaa cha Mbwa dumiani hufanyika Septemba 28 kila mwaka na Kauli Mbiu ya mwaka huu inaeleza kuwa"KICHAA CHA MBWA,KWA WOTE,AFYA MOJA KWA WOTE,".
MWISHO.
Kijana
(ambaye jina lake halikuweza kupatikana)akiwa ameleta Mbwa kwa ajili ya kupata
Chanjo ya Ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa katika viwanja vya Madeco mjini Maswa.
Mkuu
wa Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi wilaya ya Maswa,Robert Urassa akitoa
Elimu kwa wananchi(hawapo pichani)juu ya umuhimu wa kuchanja wanyama Mbwa na
Paka ili kudhibiti ugonjwa kichaa Cha Mbwa kwenye viwanja vya Madeco mjini
Maswa.
Post a Comment