Na Derick Milton, Bariadi.
Watoto wawili wa kike ambao wote ni mapacha wenye umri wa miaka 17 wanaoishi katika kijiji cha Bubale kata ya Nkololo wilayani Bariadi mkoani Simiyu wamefariki dunia kutokana na kile kinachodaiwa kupewa dawa ya kukuza matiti na mganga wa kienyeji.
Mganga huyo ambaye ni mkazi wa Byuna Wilayani humo aliyejulikana
kwa jina la Masunga Tumolo alikuwa akiwapatia dawa hiyo ya kukuza matiti ili
wapate kuolewa.
Tukio hilo limetokea jana oktoba 04, 2023 katika kijiji cha Byuna ambapo ndipo anapoishi mganga huyo.
Wananchi wa kijiji hicho wameeleza
kuwa watoto hao wamepoteza maisha katika nyakati tofauti.
Mganga mfawidhi kituo cha Afya Byuna Dkt. Deogratius Nteki amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo ameeleza leo Septemba 05, 2023 majira ya saa 10:00 Alfajiri aliletwa mtoto mmoja kati ya hao katika kituo hicho.
“ Mtoto huyo alikuwa na hali mbaya, akitapika damu, tulimpatia
huduma lakini alipoteza maisha, baadaye mwingine aliletwa naye akiwa katika
hali mbaya, katika kumpatia matibabu naye alipoteza maisha,” amesema Dkt.
Nteki.
Mganga Mfawidhi huyo amesmea kuwa chanzo cha kifo ni watoto hao
kupewa dawa inayodhaniwa kuwa na sumu alipopelekwa kwa mganga wa kienyeji kwa
ajili ya kupatiwa matibabu.
Mkuu wa Wilaya hiyo Simon Simalenga ameagiza wahusika wote
akiwemo Mganga huyo wa kienyeji, kusakwa popote walipo na hatua kali
zichukuliwe dhidi yao.

Post a Comment