RPC Simiyu ashuka vijijini kutoa elimu kukabiliana na Uhalifu, Ujangili.

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi Edith Swebe, akiongea na wa wananchi wa kijiji cha Budalabujiga wilayani Itilima (hawapo pichani) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji hapo.

 

Na Costantine Mathias, Simiyu.

 

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi Edith Swebe ameanza ziara ya vijiji kwa vijiji kwa ajili ya kutoa elimu ya kupambana na uhalifu, migogoro ya ardhi, malezi kwa vijana, kupiga vita ramli chonganishi na kuwaunganisha wananchi na jeshi hilo kupitia polisi jamii.

 

Aidha kufuatia ziara hiyo, Kamanda Swebe amewataka wananchi kuimariasha ulizni na usalama na kulinda haki za binadamu ikiwemo kukomesha mauaji na uhalifu unaondelea kwa kushirikiana na jeshi la polisi.

 

Ameyasema hayo jana (Oktoba 12, 2023) wakati akiongea na Wananchi, Viongozi wa dini na serikali, Waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala wa kijiji Budalabujiga wilayani Itilima Mkoani humo.

 

Amewataka wananchi kuhakikisha wanalisaidia jeshi la polisi ili kukomesha uhalifu na kupiga vita ukatili unaofanywa na baadhi ya wazazi au walezi vijijini.

 

‘’kuna migogoro ya ardhi inatumaliza, baba au mama anauwawa ili mtoto aweze kurithi ardhi, haya yanatoka wapi?...nimekuja kuwakumbusha kuwa maisha yana thamani lazima tuyalinde’’ amesema.

 

Amefafanua kuwa serikali imekuwa ikipoteza nguvu kazi kutokana na watu wachache wanaofanya uhalifu, huku akiwataka wananchi kuendelea kuimarisha vikundi vya sungusungu kwa kushirikiana na polisi kata.

 

Kamanda Swebe amewataka waganga wa tiba asili na tiba mbadala kutokuwa sehemu ya mauaji kupitia tiba zao huku akiwataka wananchi kuwafichua wahalifu wakiwemo waganga wa kienyeji wanaosababisha vifo.

 

Musa Kitalala, mkazi wa kijiji cha Nkoma wilayani Itilima alilipongeza jeshi la polisi kwa kutoa elimu ya ukatili, migogoro ya ardhi, pamoja na kupiga vita ramli chonganishi.

 

Naye Malugu Masanja, Mkazi wa Mitobo alilitaka jeshi hilo kushirikiana na sungusungu kuimarisha ulinzi na usalama vijijini ili wahalifu wakikamatwa wachukuliwe hatua ikiwemo kufikishwa mahakamani.

 

‘’Sijaona Kamanda wa Polisi (RPC) ameshuka kwenye kata na vijiji, hili ni jambo jipya la kumshukuru Mungu…ulinzi na usalama ulikuwa umekufa, leo umetufika, ulinzi na usalama utaimarika kwa sababu uhalifu ulikuwa unafanyika hadharani’’ Amesema Nkamba Mboje, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Itilima.

 

MWISHO.

 

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi Edith Swebe akiongea na wananchi wa kijiji Budalabujiga (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo.

 
 

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi Edith Swebe akipeana mkono na kupiga picha ya pamoja na baadhi ya wananchi baada ya mkutano uliofanyika kijiji hapo.




KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi Edith Swebe (kulia) akisamiliana na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Budalabujiga wilayani Itilima Mkoani Simiyu.

 


KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi Edith Swebe (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Budalabujiga wilayani Itilima Mkoani Simiyu.

 

 

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi Edith Swebe (kulia) akisamiliana na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Budalabujiga wilayani Itilima Mkoani Simiyu.


KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi Edith Swebe (kushoto) akiongea na wananchi wa kijiji cha Budalabujiga wilayani Itilima Mkoani Simiyu kwenye mkutano uliofanyika jana (Oktoba 12, 2023).







Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم