Wakulima wazalisha tani 278,000 za Pamba nchini.

Mkulima akikusanya Pamba kwa ajili ya kuuza.

 

Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.

 

SERIKALI kupitia Bodi ya Pamba nchini (TCA) imesema uzalishaji wa Pamba umeongezeka kutoka tani 174,000 kwa mwaka 2022 hadi kufikia tani 278,000 kwa mwaka 2023.

 

Ongezeko hilo ambalo ni sawa na asilimia 60 na kwamba limetokana na jitihada za serikali pamoja na wadau wa pamba kuhakikisha wanaboresha huduma za ugani, upatikanaji wa mbegu bora kwa wakati pamoja na wakulima kuanza kuzingatia kanuni za kilimo.

 

Akiongea na waandishi wa habari za pamba, Afisa Kilimo Mwandamizi kutoka Bodi ya Pamba, amesema kutokana na ongezeko la uzalishaji wa pamba, wakulima pia wamepata fedha nyingi na wakati huo serikali imekusanya ushuru.

 

Luneja amewataka wadau wa pamba kushirikiana na serikali kuhakikisha wanaimarisha zao la pamba, pia kudhibiti baadhi ya watu wanaochafua zao hilo kwa kuchanganya na uchafu ili kuongeza uzito.

 

‘’mwaka huu (2023) tumezalisha tani 278,000 za pamba, sawa na asilimia 60 ya lengo, tofauti na mwaka jana tulizalisha tani 174,000…niwaombe wadau wa sekta ndogo ya pamba tuendelee kushirikiana na kutoa elimu kwa wakulima’’ amesema Luneja.

 

Aidha, Luneja amesema Bodi ya Pamba inaendelea kuimarisha ufuatiliaji na usimamizi wa zao katika kilimo hai ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wawekezaji wanatoa huduma za ugani, Pembejeo, na kulipa bei ya ziada (Premium) kwa wakulima wao.

 

Kuhusu kuwepo kwa Mvua za El nino, Luneja amesema Pamba ni zao linastawi katika maeneo mbalimbali yenye miinuko na tambarare ambapo pamba hustawi hata kama kuna mvua kubwa.

 

Aidha amefafanua kuwa katika maeneo ya mbuga endapo maji yatazidi yanaweza kuathiri zao la pamba,  na endepo mvua itanyesha na kupitisha vipindi vya jua pamba haitaathirika. 

 

MWISHO.

 

 

Mkulima wa Pamba, mkazi wa kijiji cha Budalabujiga, wilayani Itilima Mkoani Simiyu akipulizia shamba lake.


Shamba la Pamba. 
 
 
 
Trekta yenye mtambo ikipakia pamba kwa ajili ya kupeleka kiwandani.






Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم