Waziri Dkt. Gwajima atoa maagizo kwa wakurugenzi nchini.

Waziri Dkt. Gwajima atoa maagizo kwa wakurugenzi nchini, akizungumza wakati wa Mkutano wa kitaifa wa wadau watekelezaji wa Programu Jumuishi ya kitaifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT MMMAM) leo jijini Dodoma. 
 

Washiriki wa mkutano wa kitaifa wa wadau watekelezaji wa Programu Jumuishi ya kitaifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT MMMAM) leo jijini Dodoma. 


Na Anita Balingilaki,Dodoma 

 

Waziri wa Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee wanawake na makundi maalum Dkt Dorothy Gwajima amewataka wakurugenzi watendaji wa halmashauri zote nchini kuhakikisha wanaweka bajeti ya utekelezaji wa programu jumuishi ya kitaifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT MMMAM) ambayo inatekelezwa kwenye mikoa yote ya Tanzania bara.

 

Maagizo hayo ameyatoa wakati akifungua  mkutano wa kitaifa wa wadau watekelezaji wa Programu Jumuishi ya kitaifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT MMMAM) leo jijini Dodoma. 

 

"Programu hii ni muhimu sana  kwa ukuaji timilifu wa mtoto na mkurugenzi atakayeshindwa kupata bajeti hiyo atakuwa anachangia sababu zinazoweza kusababisha mtoto asiweze kukua katika utimilifu wake, dugu zangu nimejaribu kujizungusha zungushaaaa, lakini nimeshindwa naomba niagize tu moja kwa moja kwamba kila halmashauri ihakikishe inapata bajeti ya kutekeleza programu hii ili ni agizo, bahati nzuri TAMISEMI wapo hapa pia wamesikia" Dkt Gwajima

 

Akimkaribisha mgeni rasmi mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka wizara ya Maendeleo ya  Jamii, Jinsia Wazee, Wanawake na Makundi Maalumu Sebastian Kitiku amesema ili kuhakikisha maeneo matano ya ECD  ambayo ni lishe, afya bora, malezi yenye mwitikio, elimu, ulinzi na usalama wa mtoto yanafanyiwa kazi kwa  uwiano huku akiongeza kuwa wizara ina mpango wa kuanza kupima maeneo hayo kwa score card.

 

Awali mkurugenzi mkazi kutoka shirika la Childrens in Crossfire Craig Ferla amesema mpaka sasa jumla ya halmashauri 70 kati ya  114  tayari  zimezindua programu hiyo huku matarajio yakiwa hadi kufikia  mwezi Marchi mwakani zote zitakuwa zimefikiwa huku  akiiomba serikali kuangalia namna ya kupata bajeti itakayosaidia utekelezaji wa programu hii kwa kasi zaidi.

 

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa klabu za waandishi wa habari Tanzani (UTPC) Kenneth Simbaya amewataka wadau wa watoto kwa umoja wao kuona umuhimu wa  kuwatumia waandishi wa habari katika shughuli zao ili kuipa jamii haki ya kupata habari/taarifa na kwa kufanya hivyo kutachochea uwajibikaji kwani waandishi ndio daraja la kuripoti ukweli na pale wanapowasema vibaya wasichukie bali wayafanyie kazi kwa kile kilichoonekana hakijakaa   vizuri kirekebishwe kwa maslahi mapana ya taifa.

 

Naye mmoja wa washiriki wa mkutano huo Janeth Ringo ambaye ni  afisa mradi wa mtoto kwanza kutoka mkoa wa Simiyu  unaotekelezwa kupitia programu ya  PJT MMMAM  amesema kupitia mkutano huo umewezesha kuongeza mbinu na namna bora ya ya utekelezaji wa programu hiyo.

 

Mkutano huo unawahusisha  maafisa ustawi wa jamii, maafisa maendeleo ya jamii, viongozi wa CSOs na waandishi vinara wa habari za watoto kutoka mikoa yote ya Tanzania bara.

 

Mkutano huo  umeanza  Disemba 11,2023 na utamalizika Disemba 14, 2023 jijini Dodoma  ukiwa na lengo la kufanya tathimini ya Programu hiyo ukienda sambamba na uzinduzi wa  mpango maalumu wa utekelezaji wa programu hiyo.

 

MWISHO.

 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم